SIFUNGI MIPAKA ,ONGEZENI TIJA - BASHE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, February 3, 2023

SIFUNGI MIPAKA ,ONGEZENI TIJA - BASHE

Na Okuly Julius-Dodoma 

Serikali imesema haitofunga mipaka yake wala kumzuia mkulima yoyote kuuza mazao yake nje ya nchi Kwa kisingizio cha kudhibiti mfumuko wa bei nchini.

Waziri wa kilimo HUSEIN BASHE ametoa msimamo huo wa serikali katika ufunguzi wa warsha ya kisheria na kisera katika mwenendo wa uzalishaji na uuzaji wa zao la tumbaku iliyofanyika jijini DODOMA

"Maadam mimi bado ni Waziri wa Kilimo sitafunga mipaka , ninachotaka ni nyie kuongeza tija katika kilimo na hapo ndipo tutaondokana na huu mfumuko wa bei kwani nani amewadanganya kuwa kufunga mipaka inapunguza mfumuko wa bei?," alihoji Bashe

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya kilimo mifugo na maji CHRISTINE ISHENGOMA amewataka wadau na wakulima nchini Kujikita katika kanuni bora za kilimo ili kuliongezea tija zao Hilo La kimkakati.

Warsha hiyo ya siku moja imewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi kutoka mkoa wa TABORA ambao ndio wazalishaji wakubwa wa zao la TUMBAKU nchini


 

No comments:

Post a Comment