TASNIA YA HABARI IPO MIKONONI MWA VYOMBO VYA HABARI MTANDAONI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, February 11, 2023

TASNIA YA HABARI IPO MIKONONI MWA VYOMBO VYA HABARI MTANDAONI


Na Okuly Julius-Dodoma 

Serekali imewataka wadau wa masuala ya habari na wamiliki wa vyombo vya habari kuzingatia weledi katika utendaji kazi wao hasa katika kipindi hiki cha Mapinduzi ya teknolojia kwa kuhakikisha wanazingatia maudhui yanayoendana na taaluma hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa  Februari 10,2023 Jijini Dodoma, wakati akizindua taasisi ya waandishi wa habari mtandaoni (TOMA) .

"Kwa sasa kinachosumbua Media house nyingi ni weledi kumeibuka na watu ambao wanazusha tu habari zao bila kuzingatia maudhui hayo yatakuwa na matokeo gani kwenye jamii ambayo ndio mlaji wa mwisho,"

"Sisi tujitahidi kujitofautisha na hao ili tulinde taaluma yetu na Serikali sio kwamba haioni juhudi za vyombo vya habari inaona na ndio maana imetoa uhuru wa kutosha kila mmoja kuanzisha na kumiliki chombo cha habari ila changamoto inatokea namna gani ya kuchuja kipi kiende hewani na kipi kisiende kulingana na maudhui yake,"amesema Msigwa 


Msigwa amesema kwa kutokana na kukuwa kwa matumizi ya TEHAMA imerahisisha habari kufika kwa jamii kwa haraka sana hivyo vyombo vya mitandaoni imekuwa tegemewe kama chanzo kikuu cha habari.

"Tasnia ya Habari ipo mikononi mwa vyombo vya habari Mtandaoni, kwa sasa vyombo vya habari Mtandaoni imekuwa nguzo kubwa kwa sekta ya habari nchini ila nitoe angalizo kwa sababu kadiri zinavyoongezeka inaonekana kama weledi wake unapungua hivyo niwatale TOMA kuhakikisha waandishi wa habari mtandaoni wanakuwa na uelewa mkubwa juu ya machapisho wanaotuma mtandaoni,"amesisitiza Msigwa 

Pia Msigwa amewataka waandishi wa habari mtandaoni kuzingatia uweledi na wasikubali kutumika na watu ama makundi yenye nia ovu kwani kukubali kutumika itapoteza ile dhana ya uwepo na ukuaji wa sekta hiyo.


No comments:

Post a Comment