WIZARA YA ELIMU YATANGAZA NAMBA MAALUMU KWA AJILI YA KUTOA TAARIFA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, February 3, 2023

WIZARA YA ELIMU YATANGAZA NAMBA MAALUMU KWA AJILI YA KUTOA TAARIFA


Na Okuly Julius-Dodoma

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeandaa kituo cha huduma kwa wateja kwa ajili ya kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi zinazohusu sekta ya Elimu.

Kituo hicho kitakuwa wazi kuanzi saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni kwa ajili ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi zihusuzo taasisi za elimu ikiwemo Shule za Msingi,sekondari pamoja na vyuo, ikiwa ni matukio yanayokiuka mila,desturi,tamaduni na miongozo mbalimbali ya Kitanzania.

Akizindua namba maalum itakayoyumika kwa ajili ya kupokelea taarifa katika kituo hicho leo Februari 3,2023 Jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wa Wizara hiyo Dkt.Francis Michael amesema kuwa mtoa taarifa atalindwa kwa mujibu wa sheria hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi badala yake watoe taarifa lengo likiwa ni kulinda watoto.

"Kimsingi kituo hichi kitakuwa kinapokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi taarifa ambazo tunaamini tukizifanyia kazi itasidia kulinda watoto na kuongeza ubora wa elimu kikubwa ni kupiga simu na kutoa malalamiko kuhusu sekta ya elimu na taarifa zako na wewe mtoa taarifa utalindwa kwa mujibu wa Sheria,"

Na kuongeza kuwa "nitaje namba hizo ambazo zitatumika kwa namba ya mezani ni 0262 160 270 na 0737 962 965 hizi ni namba ya mkononi itakuwa wazi kwanzia saa mbili kamili asubuhi mpaka saa kumi kamili jioni tayari kwa kupokea taarifa hizo kutoka kwa wanznchi," amesema Dkt.Francis

Kuwepo kwa matukio mbalimbali yanayoripotuwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kuhusu uwepo wa vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili,mila,desturi na utamaduni wa kitanzania ndio kichochoe kikubwa kilichofanya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuandaa kituo hicho cha huduma kwa wateja ili kupokea taarifa zitakazosaidia kushughulika na vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment