HAKIKA RAIS SAMIA AMETHAMINI AFYA ZA WATANZA NIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, March 20, 2023

HAKIKA RAIS SAMIA AMETHAMINI AFYA ZA WATANZA NIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Dola za Marekani (USD) 30,000,000.00 kutoka kwa Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Rais wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Mark Briston kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Elimu, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Machi, 2023. Fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa Mabweni 273 pamoja na Madarasa zaidi ya 1094 kwa Wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania

Na Mwandishi wetu Dodoma

Tanzania mikononi mwa Mama, Kauli hii inamaanisha kama taifa tunaendelea kujivunia mengi na makubwa yaliyotekelezwa na yale yanayoendelea kutekelezwa Chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ni mikaa miwili tu, Rais Samia amekamilisha ujenzi wa Zahanati 1,066, ujenzi wa Hospitali za wilaya 135, Hakuacha majengo tu akapeleka na Vifaa tiba vya kutosha.

Hatusemi ilimradi tumesema, Mama amejenga vituo vya afya 234 kupitia Tozo tu, huku vituo vya Afya 74 vimejengwa kupitia fedha za Ruzuku, na kama haitoshi kupitia mapato ya ndani vituo vya Afya 90 vimejengwa, akapeleka na vifaa tiba kwaajili ya Vyumba vya Upasuaji, Mionzi, Maabara.

Kama hiyo haitoshi Dkt. Samia ameboresha huduma za ‘AfyaMsingi’ na kuwezesha ujenzi wa majengo 80 ya dharula yaani ”EMD’’ Majengo ya kuhudumia wagonjwa mahututi yaani ICU 28, Ujenzi wa nyumba za watumishi 450

Aidha alitoa fedha za kusimika mitambo 21 ya Kuzalishia hewa safi kwa binadamu yani Oxygen, na kuajiri watumishi wa Afya zaidi ya 10,324 hii inamaanisha kwenye eneo la Afya imetumika Zaidi ya Bilioni 600 za kitanzania kwaajili ya maboresho yote.

No comments:

Post a Comment