MSD YAELEKEZWA KUPELEKA VIFAA TIBA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA WILAYA IKUNGI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, March 20, 2023

MSD YAELEKEZWA KUPELEKA VIFAA TIBA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA WILAYA IKUNGI

OR-TAMISEMI

Kamati ya kudumu ya Bunge TAMISEMI imeielekeza Bohari Kuu ya Dawa ( MSD) kupeleka vifaa tiba vilivyobaki vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Mil.129 katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Agizo hilo limetolewa Machi 19,2023 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Denis Londo baada ya kukagua utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Ikungi.

Londo amebainisha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ililipa Bohari Kuu ya dawa Shilingi Mil.300 kwaajili ya ununuzi wa vifaa tiba,baadhi ya vifaa tayari vimekwisha pelekwa lakini vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi Mil. 129 bado havijapelekwa katika hospitali hiyo.


" Ofisi ya Rais-TAMISEMI wasilianeni na MSD ili vifaa tiba vilivyobaki viletwe hapa na hiki kilichotokea hapa sio kigeni katika vituo vya afya na hospitali zetu " Amebainisha Mhe. Londo 

Aidha ameielekeza Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuhakikisha kwamba fedha iliyorudishwa hazina kiasi cha shilingi Mil. 325 kwaajili ya utekelezaji wa shughuli za afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Ikungi inarudishwe katika Hospitali hiyo ili itumike katika kuimarisha utoaji wa huduma za afya.


Sambamba na maagizo hayo Kamati imeitaka Halmashuri ya Wilaya ya Manyoni kuhakikisha ifikapo mwezi juni 2023 ujenzi wa jengo ya mochuari,wodi ya upasuaji na wodi ya kulaza wagonjwa wa kawaida uwe umekamilika.

Akihitimisha ziara ya Kamati ya kudumu ya Bunge TAMISEMI, Mhe. Londo ameitaka Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Halmashauri zote ambazo zimetembelewa na Kamati hiyo kutekeleza maagizo na maelekezo yaliyotolewa.

No comments:

Post a Comment