Na Bugoma Bugoma,Katavi
Mtoto mwenye umri wa siku mbili anusurika kifo baada ya kutupwa chooni na mama yake mzazi mara baada ya kujifungua huku chanzo kikidaiwa kuwa ni ugumu wa maisha ikiwemo kukataliwa na baba wa mtoto.
Akizungumzia tukio hilo ofisa ustawi wa Jamii halmashauri ya Nsimbo Teresia Mwendapole amesema mtoto huyo baada ya kuokolewa alipelekwa hospitali ya rufaa mkoa wa Katavi ambapo anaendelea kupatiwa matibabu.
Nao baadhi ya majirani wa kijiji hicho wamelaani tukio hilo huku wakiliomba jeshi la polisi kumchukulia hatua aliyehusika na tukio.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya watoto Hospitali ya Rufaa mkoa wa Katavi Dokta Maria Matei amethibitisha kumpokea mtoto huyo akiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake huku akieleza hali ya mtoto huyo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Ali Makame amekiri kutokea kwa tukio hilo na tayari upelelezi umekamilika ikiwa ni pamoja na jalada lake kufikishwa kwa mwendesha mashitaka wa serikali wakati mtuhumiwa akiwa nje kwa dhamana.



No comments:
Post a Comment