WAJUMBE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI TARURA WATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA MADARAJA YA MAWE SINGIDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 10, 2023

WAJUMBE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI TARURA WATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA MADARAJA YA MAWE SINGIDA


Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wamefanya ziara Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida ili kushuhudia na kujifunza Teknolojia ya ujenzi wa madaraja kwa kutumia mawe.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wametembelea daraja la mawe la Ikolo lenye urefu wa mita 30 lililopo wilayani Mkalama.

Akizungumza katika ziara hiyo Kaimu Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Edward Amboka ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kuwapatia elimu ya kutosha wajumbe wa Baraza la wafanyakazi pamoja na wahandisi wa TARURA ili kuhakikisha teknolojia hiyo inasambaa katika maeneo yote nchini.

"Hapa tupo na Mameneja wa TARURA wa mikoa yote, lengo letu ni kuhakikisha kila mkoa unaifahamu na kuitumia teknolojia hii kwani ni ya gharama nafuu", alisema Mhandisi Amboka.



Kwaupande wake Meneja wa TARURA Wilaya ya Mkalama, Mhandisi Mang'ara Matiku amesema kuwa Daraja hilo la Ikolo lilihitaji kiasi cha Sh. 550,000,000 kulijenga kwa Nondo na zege lakini kwa kutumia Teknolojia ya mawe limegharimu Sh. 180,000,000 hadi kukamilika na kuokoa kiasi Cha Sh. 370,000,000.


Naye Bi Martha Selemani mkazi wa kijiji cha Mnung'una mahali ulipo mradi huo amewapongeza wahandisi wa TARURA kwa ubunifu huo kwani wameweza kutatua changamoto ya usafiri na usafirishaji iliyokuwepo.


"Eneo hili lilikuwa halipitiki kwa muda mrefu, naipongeza Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwani kila mtu hapa anashuhudia daraja zuri na sasa tunapita kwa urahisi", alisema Martha.

Baraza la Wafanyakazi TARURA limekamilisha ziara mkoani Singida baada ya kukamilisha Mkutano wake wa tatu.

No comments:

Post a Comment