Na. Elimu ya Afya kwa Umma.
Miongoni mwa faida za Lishe bora katika maisha ya binadam ni kuwa na afya njema, hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa, huongeza uzalishaji mali na kipato na huchangia kuishi maisha marefu na yenye furaha.
Hayo yamebainishwa na Afisa Lishe wa Wilaya ya Meatu, Bi. Faustina Urassa wakati akitoa elimu ya Lishe kwenye maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji(SALiKi) katika kijiji cha mwafunguji, kata ya Kabondo, Wilaya Meatu, Mkoani Simiyu tarehe 19.03. 2023.
Elimu ya lishe imetolewa kwa wananchi 193 (wanaume 58 na wanawake 135) waliojitokeza ikijumuisha; jinsi ya kuandaa mlo kamili kwa kuzingatia makundi yote ya chakula (mapishi darasa), ulishaji sahihi wa watoto, tathmini ya hali ya lishe, usafi wa mwili na mazingira, matumizi sahihi ya chandarua umuhimu wa chanjo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Peter Mahu aliyeamtana na timu ya usimamizi wa huduma za afya kutoka Halmashauri hiyo pamoja na Viongozi wa kijiji cha mwafunguji.
Ikumbukwe kuwa, maadhimisho hayo hufanyika mara nne kwa mwaka katika kila kijiji/mtaa ikiwa ni utekelezaji wa Mkataba wa usimamizi wa shughuli za Lishe ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alisani na Wakuu wa Mikoa yote Tanzania bara mnamo tarehe 30.10.2022




No comments:
Post a Comment