RAIS RUTO ALAANI VITENDO VYA MCHUNGAJI MWENYE UTATA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, April 24, 2023

RAIS RUTO ALAANI VITENDO VYA MCHUNGAJI MWENYE UTATA


Rais William Ruto alilaani vitendo vya mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie na kuvitaja vya kigaidi wakati wa hotuba yake huko Kiambu mnamo Jumatatu, Aprili 24.

Ruto amemtuhumu Mackenzie kwa kuwapotosha wafuasi wake na kuendesha dhehebu ambalo limesababisha vifo vya watu wengi kutokana na njaa kwa ahadi kwamba watakutana na Yesu Ruto alikemea wachungaji ambao hutumia imani za kidini za kupotosha kuwanasa Wakenya wasio na ufahamu Alimlinganisha Mackenzie na gaidi, akisema kuwa anapaswa kufunguliwa mashtaka na kufungwa gerezani.


Rais William Ruto amemtaja mhubiri Paul Mackenzie kama mhalifu na gaidi kufuatia kufukuliwa kwa maiti kutoka kwa ardhi yake huko Kilifi.


Mchungaji huyo amejikuta katika upande usiofaa wa sheria na upande wa pili baada ya wapelelezi kufichua ibada yake ambayo makumi ya watu wamekufa kwa njaa kwa ahadi kwamba watakutana na Yesu.


Akiongea mjini Kiambu mapema leo, Jumatatu, Aprili, 24 Ruto ambaye alionekana mwenye hasira aliwasuta vikali wachungaji ambao wamekuwa wakitumia imani potofu za kidini kuwapotosha Wakenya.


Alimfananisha Mackenzie na gaidi na kusema anapaswa kufunguliwa mashitaka.


"Kinachoshuhudiwa huko Shakahola ni sawa na ugaidi. Mackenzie ambaye anafanya kazi ya uchungaji kwa kweli ni mhalifu wa kutisha. Magaidi wanatumia dini kuendeleza vitendo vyao viovu. Watu kama Paul Mackenzie wanatumia dini kufanya vitu kama hivi , “Watu kama hawa na magaidi wengine wowote si wa dini yoyote. Wanafaa kuwa gerezani,” Ruto alisema.


Ufukuaji wa miili waingia siku ya nne Shakahola

Rais aligusia suala hilo wakati shughuli ya ufukuaji wa miili ikiingia siku ya nne leo. Wapelelezi wa Kaunti ya Kilifi kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai bado wamekita kambi katika msitu wa Shakahola huko Malindi kutafuta miili ya wafuasi wa mchungaji Paul Mackenzie waliozikwa kwenye makaburi ya halaiki.

Chanzo Tuko.co.ke

No comments:

Post a Comment