Na Okuly Julius-Dodoma
Ackson Ameyasema Hayo Mei 18,2023 Alipotembelea Maonesho Ya Mabanda Hayo yanayofanyika katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
Amesema Amefurahishwa Na Maonesho Hayo Hususani Suala La Anwani za Makazi ambalo lilianza Mwaka Jana 2022 na Hadi Sasa limeweza kufikia Sehemu pazuri.
"Nitumie Fursa Kuwapongeza Kwa Juhudi Mbalimbali Wizara Hii Kwa Juhudi mnazozifanya Kwa Sababu Mtu Kujua Anwani yake Ni Jambo la Msingi" Amesema Ackson.
Spika Huyo Amesema Kwa wale Wananchi ambao Mpaka Hivi Sasa Bado Hawajajisajili au Hawajasajili Makazi Yao kwenye Mfumo Wa Anwani ya Makazi ni Muhimu Sana Kupata Anuani za Makazi Kwani zinasaidia kwenye Maendeleo.
"Anwani Zinasaidia Mtu kukufikia Kwa Urahisi Na Pia Zinakusaidia wewe kama Kuna Jambo umeagiza Mahali Basi Unaweza kumwambia Mtu uko Wapi na Unaishi Wapi" Amesema Spika Huyo.
Aidha, Ackson Amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Kwa Hatua walizozichukua Juu Ya Mkongo Wa Taifa Kwa Kuhakikisha Wananchi wanapata Huduma za Mkongo Hadi Majumbani.
"Naamini Mkongo Wa Taifa utapunguza Gharama za matumizi ya Bando ambayo Huwa Tunalalamika hapa Na Pale, Mnaweza Kufanya hilo Kwa Urahisi Zaidi" Amesema Ackson.
No comments:
Post a Comment