HAKUNA UPENDELEO KATIKA UTOAJI WA AJIRA MPYA: NDEJEMBI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 17, 2023

HAKUNA UPENDELEO KATIKA UTOAJI WA AJIRA MPYA: NDEJEMBI


OR TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Deo J. Ndejembi amesema ajira mpya za kada ya Ualimu 13,130 zilizotangazwa na Serikali zitatolewa kwa kuzingatia vigezo vilivyotolewa katika tangazo la ajira na hakutokuweo upendeleo Maalum kwa Walimu Wanaojitolea.


Ameeleza hayo Bungeni Dodoma wakati alijibu Swali la nyongeza la Mhe. Daniel Baran Sillo, Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini aliyetaka kujua kuna mpango wa kutoa kipaumbele kwa Walimu wanaojitolea katika halmashauri ya Babati.


“Ajira mpya zitatolewa kwa usawa, hakutakuwepo upendeleo maalum ambao utatolewa kwa Walimu wanaojitolea ili kutoa fursa sawa kwa walioomba nafasi hizo, nafasi zitatolewa kwa wanaokishi vigezo vilivyotolewa katika tangazo la ajira”


Wakati akijubu Swali la Msingi lilouliza Je, ni lini Serikali itapunguza tatizo la upungufu wa Walimu katika Shule za Sekondari Babati Vijijini
 

Ndejembi amesema Serikali imeshaanza kupunguza tatizo la upungufu wa Waalimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati ambapo katika mwaka wa fedha wa 2021/22, walimu 50 walipelekwa katika shule zilizopo Babati Vijijini.


Aidha, Ndejembi amesema katika Mwaka wa Fedha 2022/23, Serikali imetangaza nafasi 13,390 za ajira kwa waalimu ambapo baadhi ya walimu hao watapangiwa katika Shule zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati.


Amesema Serikali itaendelea kuajiri walimu na kuwapeleka katika Shule zote nchini hususan katika maeneo yenye uhitaji kadri ya upatikanaji wa fedha.

No comments:

Post a Comment