Na Mwandishi wetu -Dodoma
Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Mei 26, 2023 jijini Dodoma akilishamwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango katika uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa katika kutekeleza hilo, Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliagiza zitengwe fedha katika Mradi wa HEET kwa ajili ya kufadhili masomo ya wahadhiri walioajiriwa kwenye vyuo vikuu binafsi ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu vinavyomilikiwa na taasisi za dini.
"Katika kutekeleza agizo la Rais wetu tumetenga jumla ya dola za kimarekani milioni moja kwa ajili ya kufadhilia masomo ya wahadhiri kutoka Vyuo Vikuu Binafsi katika Shahada za Uzamili na Uzamivu" amesisitiza kiongozi huyo
Prof. Mkenda ameongeza kuwa mpaka sasa wahadhiri 27 wa vyuo vikuu binafsi wamenufaika na ufadhili huo, huku Chuo Kikuu cha Mtakatifu John nacho kikinufaika ambapo wahadhiri wake watatu wanasomeshwa katika ngazi Shahada za Uzamivu nje ya nchi.
Waziri Mkenda amekitaka Chuo Kikuu cha Mtakatifu John kuendelea kupanua zaidi uwezo wa kudahili kwa kuimarisha ubora wa mafunzo na kuongeza miundombinu ya chuo.
Aidha, amevitaka vyuo vikuu vyote nchini kuhakikisha vinasimamia ubora wa elimu inayotolewa ili kuzalisha wataalamu mahiri wenye weledi na kuwataka Wahadhiri kujikita katika kufanya utafiti.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Yohana Msanjila amesema juwa Chuo hicho kilikuwa na changamoto ya ofisi kwa watumishi na kupelekea wanataaluma ambao ni wakuu wa idara kuchangia ofisi kinyume na taratibu za usimamizi wa vyuo vikuu, hivyo changamoto hiyo ndo iliyotoa msukumo wa kufikia uamuzi wa kujenga jengo hilo la utawala
Prof. Msanjila ameongeza kuwa jengo hilo lenye vyumba vya ofisi 33, kumbi za mikutano mbili, sehemu za kupumzikia tatu na jiko limegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja na miliioni mia tisa mpaka kukamilika kwake.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha St. John's Prof. Penina Mlama amesema chuo hicho kimekuwa na mchango mkubwa katika kutoa elimu ambapo mpaka kimeshatoa wahitimu 10002
Prof. Mlama amemhakikisha Waziri Mkenda kuwa chuo hicho kitaendelea kutoa mchango kwa taifa kwa kuandaa wataalamu katika fani mbalimbali.
No comments:
Post a Comment