TUZINGATIE KANUNI ZA USAFI KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 25, 2023

TUZINGATIE KANUNI ZA USAFI KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO.


Na.Elimu ya Afya kwa Umma

Jamii imeaswa kuendelea kuzingatia kanuni za afya ikiwa ni pamoja na kuyaweka mazingira katika hali ya usafi ili kujikinga na Magonjwa ya Mlipuko.


Rai hiyo imetolewa na Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Dkt.Kisaka Deo mara baada kufanya ziara katika visiwa vya Goziba, Kerebe na Nyaburo vilivyo ndani ya ziwa Victoria kwa ajili ya kujionea namna elimu ya afya ilivyozaa matunda katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika visiwa hivyo ikiwemo Marburg kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja UNICEF na MV Jubilee Hope Medical Ship Program chini ya Kanisa la AIC Tanzania.



Dkt.Kisaka amesema ni muhimu kuweka mazingira katika hali ya usafi katika kujikinga na magonjwa ya mlipuko.


“Ili kujikinga na Magonjwa yote lazima tuyaweke mazingira yetu katika hali ya usafi,unaponawa mikono haujikingi na Marburg pekee inasaidia pia kwa kujikinga na magonjwa kama vile kuhara,Kipindupindu, kuumwa tumbo “amesema.


Katika hatua nyingine Dkt. Kisaka amehimiza akina mama wajawazito kubadili tabia na kuwa na desturi ya kuwahi kliniki mapema pamoja na kuwapeleka watoto kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kupata chanjo mbalimbali.



Kwa upande wao baadhi ya viongozi katika visiwa hivyo akiwemo Afisa Mtendaji kata ya Kerebe Kanali Sefu Muya, diwani kata ya Kerebe Sudy Said Self pamoja na diwani kata ya Goziba Mataba Mataba wakazungumzia namna serikali ilivyochukua hatua katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.


“Maelekezo ya mara kwa mara serikali imekuwa ikiyatoa hawajatuacha nyuma ,kwa kweli Wizara ya Afya naishukuru licha ya mazingira magumu ya kufikika huku lakini wataalam wamekuwa wakifika na kutoa maelekezo na baada ya elimu kutolewa mpaka sasa hatujapata mhisiwa yeyote na watu wanaendelea kuchapa kazi kama kawaida”amesema Kanali Sefu Afisa Mtendaji Kata ya Kerebe.



“Mhe.Rais amefanya jambo la maana sana kutuangalia na sisi wa huku visiwani baada ya ugonjwa huu kujitokeza kulikuwa na mshituko mkubwa lakini nashukuru wataalam wa Afya kutoka Wizarani, Mkoani kwa kweli walifika kwa wakati wametoa semina na vifaa mbalimbali vya kinga ikiwemo ndoo na vitakasa mikono “amesema Sudy Said diwani kata ya Kerebe.


“Tunaishukuru sana serikali kwa kutuma timu ya wataalam kwa awamu ya kwanza sasa ya pili kuja kutuangalia ,sisi wananchi wa Goziba tumekuwa na tahadhari juu ya magonjwa ya mlipuko hii ni kutokana na elimu ya afya kutolewa katika maeneo haya ikiwemo umuhimu wa maji maji tiririka”amesema Mataba Mataba diwani kata ya Goziba.



Nao baadhi ya wananchi kutoka visiwa wameishukuru serikali kwa kuondoa hofu na tahaharuki na kujikita zaidi utoaji wa elimu ya afya hali ambayo imesabibisha kuzingatia kanuni za afya na kuendelea na shughuli za kila siku.


“Muendelee kutuelimisha msituchoke kutuelimisha zaidi”amesema Peter Mkonjwa Msimamizi wa mwalo wa kisiwa cha Nyaburo -Beach Management Unit(BMU).


“Nashuku maana kila wataalam wa afya wanapokuja wanatuelimisha somo la afya linatuingia kichwani, tunazingatia usafi katika kuhakikisha tunajikinga na magonjwa ya mlipuko”amesema Mary Josephat mkazi wa kisiwa cha Nyaburo.



Ikumbukwe kuwa jumla ya wanajamii 89 ,viongozi viongozi 3,Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii(CHW) 6 walifikiwa katika kisiwa cha Goziba huku wananchi 161,wanafunzi 124 shule ya Msingi wakifikiwa kupatiwa elimu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko katika kisiwa cha Kerebe .


No comments:

Post a Comment