Na Okuly Julius-Dodoma
Akiwasilisha Hotuba ya utekelezaji wa vipaumbele vya Bajeti vya mwaka 2022/23 na vipaumbele vya mwaka vya mwaka 2023/24, leo Mei 31,2023 Bungeni jijini Dodoma,Waziri wa Nishati Mhe.January Makamba amesema katika fedha hizo walizoomba kuidhinishiwa na Bunge kwa mwaka 2023/24 jumla ya Trillioni 3.04 zitagawanywa katika sehemu mbili kimatumizi.
Mhe.Makamba amesema kuwa ,Sehemu ya kwanza ya Bajeti hiyo ambayo ni Zaidi ya shilingi Trilioni 2.96 sawa na asilimia 97.1 ya Bajeti yote itatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo Zaidi ya Shilingi Trillioni 2.60 ni fedha za ndani na zaidi ya shilingi Bilioni 351.5 ni fedha za nje.
Sehemu ya pili ya Bajeti hiyo zaidi ya shilingi Bilioni 87.92 sawa na asilimia 2.9 ya Bajeti yote itatumika kwa ajili ya matumizi ya kawaidi ambapo Zaidi ya shilingi Bilioni 71.63 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC) na Zaidi ya shilingi Bilioni 16.29 kwa ajili ya Mishahara (PE) ya watumishi wa Wizara na Taasisi zilizopo chini yake.
No comments:
Post a Comment