Na Okuly Julius Dodoma
Naibu Waziri wa maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amezindua Mradi wa Majisafi eneo la Ntyuka Chimalaa Leo Juni 1,2023 Jijini Dodoma.
Mhe.Mahundi amesema kuwa kazi kubwa ya Wizara ya Maji ni kuhakikisha dhamira ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Dkt.Hamia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo Kichwani inafanikiwa Kwa asilimia 100.
Mhe.Mahundi akimuwakilisha Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso katika Uzinduzi huo ameitaka Mamlaka ya Majasafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kufikisha maji katika Zahanati ya Ntyuka ili kuhakikisha huduma ya maji inapatikana lengo likiwa ni kuepusha Magonjwa ya Mlipuko.
"Dhamira ya Dkt.Samia ni kuhakikisha huduma ya maji inafika kwa asilimia 100 katika maeneo ya yanayotoa huduma za kijamii ikiwemo kwenye vituo vya Afya hivyo basi Mkurugenzi Wa DUWASA nakuagiza kahakikishe huduma ya maji inafika kwenye Zahanati ya Ntyuka,"amesema Mhe.Mahundi
Awali akitoa Taarifa ya Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majasafi na Usafi wa Mazingira (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph,amesema kuwa Mradi huo utawanufaisha wakazi zaidi ya 4,441 katika maeneo ya Ntyuka mtaa wa Chimalaa na Nyerere ambao Kwa sasa watapata maji Kwa asilimia 97 kutoka asilimia 0 ya awali.
Mhandisi Aron amesema gharama za Mradi huo Kwa awamu ya kwanza mpaka kufikisha maji Kwa wananchi ambao ndio walengwa imefikia zaidi ya Shilingi Milioni 471.8
No comments:
Post a Comment