HATUHITAJI MAMLUKI MICHEZO YA UMITASHUMTA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 3, 2023

HATUHITAJI MAMLUKI MICHEZO YA UMITASHUMTA


Angela Msimbira TABORA

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Dkt. Charles Msonde amewataka wasimamizi wa michezo ya Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) kufuata miongozo ya kutokuwa na Mamluki katika michezo hiyo


Akiongea na baraza la michezo la UMITASHUMTA leo juni 3, 2023 kwenye viwanja vya michezo ya shule ya Sekondari ya wavulana Tabora, Mkoani Tabora amesema miongozo ya michezo inasema ili mtoto kushiriki mashindano ya UMITASHUMTA anapaswa anapaswa kuwa na umri usiozidi miaka 14 kinyume na hapo ni uvunjaji wa sheria, kanuni na taratibu ya miongozo iliyowekwa.


“Watoto wanapokuja kuanza darasa la wanza wakiwa na miaka 6 ukikaa ndani ya miaka saba shuleni hautazidi miaka kumi na nne Kumekuwa na maneno kuwa wanafunzi wa MEMKWA wanaumri zaidi ya miaka 14 ndio maana muongozo unamtaka mshiriki wa michezo hiyo asiwe zaidi ya miaka kumi na nne” amesisitiza


Amewataka viongozi wanaosimamia mashindano hayo kuhakikisha wanawarejesha wanamichezo wasio na sifa iwapo watabainika kwa kuwa lengo la serikali ni kujenga timu ya shule za msingi kuanzia mika 6 hadi mika 14.


“Watumishi wenzangu tupo kazini, na kwa kuwa tupo kazini tuzingatie kanuni, sheria na taratibu za utumishi wa umma na hampaswi kufanya mambo mengine yaliyopo kinyume na taratibu na miongozo ya kiutumishi” amesisitiza Dkt.Msonde


Amewataka watumishi hao kuhakikisha wanaongoza michezo ya UMITASHUMTA ikiwa ni pamoja na kusimamia usalama wa watoto ambalo ndilo jambo muhimu, ili waanze na kumaliza michezo wakiwa salama kama walivyokuja


Amesisitiza kuwa michezo ni taaluma hivyo uzingatiaji wa kanuni, taratibu na miongozo ya kitaaluma vinapaswa kupewa kipaombele kama yanavyopewa masomo mengine shuleni.


Aidha, Dkt. Msonde amewataka kuacha tabia ya kuingiza wachezaji wasio na sifa kwenye kundi la watu wenye ulemavu kwa kuwa lengo la michezo ni taaluma hivyo iende katika misingi ya miongozo iliyopo.

No comments:

Post a Comment