Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende ametoa wito kwa Mawakili wote nchini kushiriki maadhimisho ya miaka mitano ya Ofisi ya wakili mkuu wa serikali yatakayo ambatana na mafunzo kwani ni fursa adhimu na ya kipekee.
Dkt. Luhende ameyasema hayo leo Juni 1,2023 Jijini Dodoma wakati akizungumza na wandishi wa habari kuelekea maadhimisho hayo ambapo yatafanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete kuanzia Juni 6-8 huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa.
Aidha ameongeza kuwa katika maadhimisho hayo kutakuwepo na maonesho mbalimbali kupitia mabanda yaliyo andaliwa lengo likiwa ni kuonesha namna wanavyotekeleza wajibu wao.
“Kutakuwepo na wakufunzi wabobevu walio alikwa yaani majaji waliopo kazini na wastaafu, majaji wa mahakama kuu, rufaa, wataalamu wa sheria na wakufunzi wa vyuo watatoa mafunzo kwa Mawakili,”amesema Dkt. Luhende.
Amesema kauli mbiu katika maadhimisho hayo ni “Tulipotoka, tulipo na tunapoenda”.
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ilianzishwa Februari 13,2018 kupitia hati hidhini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyotolewa kwa mujibu wa ibara ya 36 ibara ndogo ya kwanza ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na kutangazwa katika gazeti la serikali namba 50 la 2018.
No comments:
Post a Comment