MITAZAMO HASI KATIKA JAMII CHANZO CHA WANAWAKE KUSHINDWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UONGOZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 17, 2023

MITAZAMO HASI KATIKA JAMII CHANZO CHA WANAWAKE KUSHINDWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UONGOZI


Na Asha Hassan ,Dodoma

Mtandao wa kijinsia Tanzania TGNP Umetoa Mafunzo ya kuwajengea uelewa wanahabari wa vyombo vya Habari vya kijamii wa Mkoa wa Dodoma kuandika Taarifa zenye mlengwa wa kijinsia ambazo zitaondoa mitazamo hasi juu ya mwanamke katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii.


Akieleza malengo ya mafunzo hayo Mratibu wa mafunzo kutoka TGNP, CATHERINE MZURIKWAO, amesema TGNP, imeandaa mafunzo hayo ya siku mbili Kwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa waandishi wa habari kuandika habari zenye mlengwa wa kijinsia ambazo zinaweza kuchochea na kuhamasisha wanawake kugombea nafasi mbalimbali katika jamii.


DKT.ANANILEA NKYA, yeye ni mwezeshaji wa mafunzo hayo anasema,Waandishi wa Habari wananafasi kubwa katika jamii Kuondoa mitazamo hasi iliyopo kwenye jamii juu ya mwanamke ambayo inamkandamiza mwanamke katika kugombea nafasi mbalimbali katika jamii


"Kama tutaweza kuandika habari za kuwainua wanawake katika masuala ya uongozi tutaweza kuleta mabadiliko chanya katika jamii inayowazunguka kwakuwa mwanamke anasifa kuu ya uongozi ambayo ni uoga hivyo hataweza kutumia vibaya uongozi wake" alisema ANANILEA.



Brighton kimaro mwanahabari kutoka wilaya ya kondoa amesema amefurahi kupata nafasi hiyo mafunzo atakayoypata yatamsaidia katika kumjengea uwezo wa kuandaa habari zinazohimiza wanawake kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo uongozi.


Naye Elizaberth Paulo Mwanahabari kutoka Msumba News Blog amesema mafunzo hayo yamefika Kwa wakati muafaka kama Mwanahabari ataweze kufikisha Elimu katika jamii ikiwa ni kwa kuandaa makala na kufanya habari mbalimbali zinazohusu wanawake na uongozi.


 SAIDA ISSA , Mwanahabari wa gazeti la Zanziba Leo , anasema Mitazamo hasi katika jamii imekuwa kikwazo kikubwa Kwa wanawake wengi kuchangamkia fursa mbalimbali za uongozi Kwa kuwa ni nikandamizi kwake hivyo akiwa mwandishi wahabari anajukimu kubwa na kuhakikisha jamii inaondoa mitazamo hasi na kumuona mwanamke.

No comments:

Post a Comment