Na Okuly Julius-Dodoma
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Anthony Mavunde amewataka wafanyabiashara na wananchi kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadha na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutokomeza mifuko ya plastiki na kuhifadhi mazingira.
Mhe.Mavunde ameyasema hayo Leo Juni 2,2023 Jijini Dodoma,wakati akizungumza baada ya Zoezi la Usafi wa Mazingira ikiwa ni muendelezo wa wiki ya Maadhimisho ya Usafi wa Mazingira duniani ambayo Kilele chake ni Juni 5,2023.
Ambapo Mhe.Mavunde amesema kuwa suala la Usafi na utunzaji wa Mazingira ni endelevu sio la siku Moja hivyo wananchi wasisubiri mpaka Maadhimisho yafike ndio waanze kufanya Usafi na kutunza Mazingira.
"Usafi na utunzaji wa Mazingira ni muhimu kufanyika Kila siku ni suala endelevu tusitegemee tu Maadhimisho yafike ndio tuanze hili liwepo ndani ya mioyo yetu tutunze Mazingira nayo yatatutunza,"
Na kuongeza kuwa"Niwatake wafanyabiashara na wananchi kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadha na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutokomeza mifuko ya plastiki na kuhifadhi mazingira,"amesema Mhe.Mavunde
Pia Naibu Waziri huyo amesema kuwa Dodoma kama Makao Makuu ya nchi panatakiwa kuwa Mfano katika Kila kitu na anaamini kwa Kasi iliyopo Kwa sasa ya Serikali ya awamu ya Sita Inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan Dodoma inakwenda kuwa Kinara katika Usafi wa Mazingira.
"Ukitembelea miji mikuu katika nchi nyingine utaona tofauti kubwa sana na sisi kwani ili uwe mji Mkuu lazima uongoze katika maeneo muhimu ikiwemo eneo la Usafi wa Mazingira na ndipo Dodoma tunapoelekea ni lazima tuwe Kinara katika Usafi na Uhifadhi wa Mazingira,"Ameongeza Mhe.Mavunde
Adha,ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Chini ya Dkt.Suleiman Jafo Kwa kazi kubwa wanyoifanya ya kuhakikisha agenda ya Usafi na utunzaji wa Mazingira inafanikiwa.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe.Godwin Gondwe amesema kuwa Dodoma imeamua kubeba kikamilifu agenda ya Usafi na utunzaji wa Mazingira na dhamira ya Serikali inafanikiwa.
"Dodoma hatutapoa katika utunzaji wa Mazingira tutaendelea kuhamasishana na wananchi wa Jiji la Dodoma kutunza na kuhifadhi Mazingira,"amesema Gondwe
Naye Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt.Switbert Mkama amesema Maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika Kwa kufanya Usafi katika Mitaa mbalimbali ya Jiji la Dodoma.
Kilele cha maadhimisho ya wiki ya mazingira Kitaifa itanyika Juni 5,2023 ,Mgeni Rasmi akitarakiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango na yatafanyika Jijini Dodoma eneo la Soko la Machinga.
No comments:
Post a Comment