SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA ELIMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, July 10, 2023

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA ELIMU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akiweka jiwe la Msingi Katika shule ya Msingi Muungano iliyopo katika kijiji cha Namatuhi kata ya Ndongosi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Halmashauri ya Songea Vijijini Ndg. Thomas Simon Masolwa wakati wa mkutano wa hadhara Uliofanyika katika Kitongoji cha Muungano.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akizungumza jambo Diwani wa Kata ya Ndongosi Mhe. Zakaria Mbilinyi wakati wa mkutano wa hadhara Uliofanyika katika Kitongoji cha Muungano.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akicheza ngoma za kitamaduni na wakinamama wa kijiji cha Namatuhi wakati wa Ziara yake katika kata ya Ndongosi.


Na Mwandishi wetu Ruvuma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho amesema Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI itajenga vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Muungano iliyopo Halmashauri ya Songea.


“Tunataka kufanya ukarabati Madarasa na kujenga mengine ili shule ya Msingi Muungano iwe miongoni mwa shule za mfano kwa kuwa na Miundo Mbinu Bora ya Elimu”.


Kauli hiyo ilitolewa tarehe 9/07/2023 katika Kijiji cha Namatuhi Kata ya Ndongosi Halmashauri ya wilaya ya Songea Wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi wa ujenzi wa Vyumba Viwili vya Madarasa vinavyomaliziwa kujengwa.


Waziri Mhagama, ameelekeza watendaji wa Halmashauri ya wilaya kuhakikisha hatua ya umaliziwaji wa ujenzi wa vyumba hivyo viwili vya madarasa uwe imekamilika ndani kipindi cha wiki Mbili.


Akizungumzia kuhusu uharibifu wa Misitu na vyanzo vya maji Waziri Mhagama amewaomba Wananchi wa kijiji cha Namatuhi kuendelea kuhifadhi mazingira na kuepuka tabia ya ukataji wa miti.


Amesema chanzo cha maji cha Kitinginyi ndio chanzo pekee kilichobaki, kinapaswa kulindwa ili kuepusha shughuli nyingine za kibinadamu zinazoweza kuharibu chanzo hicho cha maji.


“Tuendelee kutunza chanzo hicho cha maji kwa kupanda miti ili huduma ya maji iweze kunufaisha vijiji vingine vya jirani,” alisema Waziri Mhagama.


Kwa upande wake Mkugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mwalimu Neema Magembe amesema gharama za ujenzi wa Vyumba Viwili vya Madarasa mpaka ujenzi ulipofikia ni shlingi Millioni 34.


Ameongeza kusema, Halmashauri tayari imeshaweka fedha za umaliziaji wa vyumba hivyo madarasa kwa kuweka Marumaru.


Awali Diwani wa Kata ya Ndongosi Mhe. Zakaria Mbilinyi amemshukuru Waziri Mhagama kwa kutuma Mhandisi wa maji ambaye alifanya utafiti na kugundua chanzo cha maji katika kitongoji cha Muungano kilichopo katika Kijiji cha Namatuhi kata ya Ndongosi.


“Wananchi wanamatumaini Makubwa, kwamba watapata huduma ya maji safi na salama alisema,” Mhe. Mbilinyi.

No comments:

Post a Comment