WADAU WA SEKTA YA MAJI NA UJENZI WASHAURIWA KUSHIRIKIANA NA GST KWENYE MIRADI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, July 29, 2023

WADAU WA SEKTA YA MAJI NA UJENZI WASHAURIWA KUSHIRIKIANA NA GST KWENYE MIRADI


GST - Dodoma.

Mkuu wa Mkoa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka wadau wa sekta ya maji na ujenzi mkoani Dodoma kushirikiana na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) juu ya kutumia taarifa za tafiti za maji na miundombinu ya ujenzi zinazofanywa na GST.


Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wakati akipokea ramani inayoonesha jiolojia ya Dodoma na kitabu cha madini yapatikanayo Tanzania kuanzia ngazi ya Kijiji Kata Wilaya mpaka Mkoa toleo la tano.


Akisisitiza juu ya ushirikiano huo Senyemule amewashauri wadau wa sekta ya maji na ujenzi washirikiane na GST kwa kuwa wanaonesha kuwa na vifaa vya kisasa vya utafiti na uchunguzi pamoja watalaamu wenye uzoefu kuhusiana na masuala la jiolojia.



Akifafanua juu ya kitabu hicho na ramani hiyo meneja wa sehemu ya jiolojia GST Maswi Solomon alisema taarifa za jiolojia zinazotolewa na GST sio zile zilizojikita kwenye madini pekee bali hata kwenye tafiti za maji na majanga ya asili ya jiolojia ikiwemo tathmini ya maeneo ya ujenzi wa miondombinu mbalimbali kama vile ujenzi wa majengo marefu.


Akifafanua wakati wa uwasilishwaji wa Kitabu hicho Maswi alifafanua kuwa Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa Mikoa inayohitaji maji ya ardhi kutokana na ukweli kuwa ndio chanzo kikuu kwa sasa cha kuweza juhudumia wananchi na hivyo kuhusisha chanzo hicho cha maji na taaluma ya jioloji.


Lengo kubwa ni kubaini nyufa zinazohifadhi maji chini ya ardhi kupitia utafiti wa jiofizikia ambao ni muhimu pia kushauri hali ya maji (chumvi/baridi) kupitia utafiti kwa njia ya umeme.


Kwa upande wa majanga ya asili ya jiolojia utafiti kwa njia ya jiofizikia ni muhimu kubaini nyufa au mipasuko chini ya ardhi zinazoweza kuathiri uimara wa majengo marefu na mazito hivyo kushauri Sekta ya ujenzi na maji kwa pamoja kushirikiana na GST ili kutafiti chini ya ardhi.


Maswi aliongeza kuwa kwa sasa Taasisi kadhaa za Serikali zinazo jenga majengo Dodoma zimeanza kutumia taarifa za GST kama msingi wa kuanza kuendeleza miradi ya ujenzi hivyo kuomba na Sekta binafsi kuona umuhimu wa kufanya hivyo kwa kuwa hakuna sheria inayowalazimisha kufanya hivyo kwa sasa bali wazingatie usalama na uimara wa majengo yao.

No comments:

Post a Comment