OR-TAMISEMI, Kibaha
Mratibu wa Kituo cha Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) Shwaibu Hussein amesema washiriki 172 katika kituo cha Halmashauri ya Mji wa Kibaha wamenufaika na mafunzo hayo yanayokwenda kuleta mabadiliko kwenye elimu.
Shwaibu ameyasema hayo Julai Mosi, 2023 wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Elimu ya Awali, Walimu Wakuu na Maafisa Elimu Kata kuhusu Njia na Vifaa vya Mtaala wa Elimu ya Awali Vilivyoboreshwa, yanayotolewa kupitia Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Ujifunzaji Elimu ya Awali na Msingi(BOOST).
Amesema idadi yote iliyotakiwa kushiriki wameshiriki hali hiyo inatoa taswira kuwa mafunzo yanayoendelea kwa walimu yataenda kuleta mabadiliko katika elimu.
Naye, Mshiriki wa mafunzo hayo, Mwalimu Rosa Mlali ameishukuru Serikali kuwezesha mafunzo hayo na kushauri yawe endelevu kwa walimu ili kusaidia kupata maarifa na ujuzi mpya na kuwaongezea kujiamini katika ufundishaji wao.
No comments:
Post a Comment