![]() |
Meneja wa Agricom kanda ya Kati na Kaskazini Peter Temu akiongea na waandishi wa habari katika maonesho ya nanenane 2023 |
![]() |
dhana mpya ya kilimo ya Trekta aina ya KUBOTA yenye twowill na fourwill kwa wakati mmoja inayosambwaza na Agricom Afrika. |
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Kampuni ya Agricom inayojishughulisha na usambazaji wa dhana za kilimo katika maonesho ya Nanenane 2023 wamekuja na Trekta aina ya KUBOTA yenye matumizi rafiki kwa wakulima kwa kutumia mafuta kidogo pamoja na kuwa na fourwill na twowill kwa wakati mmoja tofauti na trekta zingine.
Akiongea na waandishi wa habari katika maonesho hayo kanda ya Kaskazini yanayoendelea mkoani Arusha Meneja wa Kanda ya Kati na Kaskazini wa Agricom Peter Temu alisema uwezo wa trekta hiyo ni sawa na uwezo wa kutumia trekta mbili za aina nyingine kwa mara moja ambayo inauwezo wa kufanya kazi mahali popote kilingana na aina ya udogo.
Alieleza kuwa matengemeo yao ni kuwasaidia wakulima wa Kanda ya Kaskazini waweze kufanya vizuri kwenye kilimo chao kwaniTrekta hiyo ina ubora mkubwa kwenye matumizi ya mafuta lakini pia urahisi katika upatikanaji wa vipuri.
“Ukiwa na Trekta hii ni sawa na kuwa na Trekta mbili kwa wakati mmoja kwasababu Trekta zingine zilizopo sokoni hazina twowill na fourwill kwa wakati mmoja, na kwa mazingira ya Tanzania Trekta hii unaweza kuifanyia kazi mahali popote,”Alisema.
Alifafanua kuwa kutokana na utendaji mkubwa wa Trekta hiyo wakulima watarajie kupata faida kubwa kutokana na walichokifanya kutokana na kwamba teknolojia hiyo ni ya Japan na inasambazwa na Agricom peke yake ambao wanajali kazi za mkulima kwaanzia kuandaa shamba hadi anapohifadhi mazao yake.
“Tunachofanya Agricom ni kutathimini jinsi wakulima wanavyoweza kupata faida zaidi kwa kuwasambazia dhana bora kwanzia uaandaaji wa shamba hadi anapofikia kuhifadhi mazao yake, lakini pia kumuinua kutoka kwenye dhana za zamani na kuja kwenye dhana za kisasa zinazoleta tija zaidi,” Alieleza.
“Trekta hii aina ya KUBOTA ililetwa maalum baada ya kufanya tathimini kubwa ya matumizi ya dhana bora za kilimo, hii ina silinder nne na cc 2000 ambayo ni ndogo sana na inawezesha matumizi kidogo ya mafuta ambapo ikiwa kwenye fouwill itatumia lita tatu hadi nne wakati zingine zitatumia lita tano hadi saba,”Alifafanua.
No comments:
Post a Comment