Dkt. Kijaji ameyasema hayo Agosti, 3 2023 alipokua akizungumza na wafanyabiashara Jijini Tanga kwa lengo la kusikiliza changamoto zao za kibiashara na kuzitafutia ufumbuzi.
Aidha, amebainisha kuwa Dhamira ya Serikali nikulirudisha jiji la Tanga kuwa jiji la Viwanda nchini kama hapo awali ili liweze kutoa ajira kwa vijana kukuza biashara na uchumi wa Taifa .
Vilevile, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeamua kukabidhi uchumi katika sekta binafsi ili uchumi uwe imara ndani na nje ya Nchi.
Dkt. Kijaji pia ameishauri TRA isiwabebeshe mzigo wafanyabiashara kwa kulimbikiza kodi bali ameitaka TRA ishirikiane na wafanyabiashara hao na kuwapa elimu kuhusu ulipaji kodi ili kukuza uchumi.
No comments:
Post a Comment