Na Okuly Julius-Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki amewataka waweka hazina na wahasibu kuwafutilia Mawakala waliopewa dhamana ya kukusanya Mapato katika Halmashauri ili kuziba mianya ya upotevu wa mapato.
Mhe. Kairuki ameyasema hayo leo Agosti 17,2023 Jijini Dodoma katika kikao kazi cha ukaguzi wa hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha na waweka hazina na wahasibu wa sekretarieti za mikoa na mamlaka za Serikali za mitaa ambapo amesema kumekuwa na changamoto kubwa hasa kwa maafisa wahidhiniwa na mawakala wanao kusanya mapato kwa niaba ya halmashauri.
"Pengine unaweza kukuta ni wezi au hawana historia nzuri halafu hatujachunguza na tunakuja kuwapa madaraka makubwa ya kufanya kazi kwa niaba ya halmashauri, kwa hiyo ni vyema nanyi mkaanza kufuatilia kuangalia kila chanzo,"amesema Mhe. Kairuki.
Aidha, ameongeza kuwa ni vyema wakaangalie tena vigezo wanavyotumia kuwapata mawakala hao pale wanapohitajika pamoja na kuangalia historia zao katika masuala ya kifedha.
"Wapo ombao wamepewa mashine za kukusanyia mapato lakini unakuta wengine wanazo mbili mbili, na yawezekana wengine tunawajua ni vyema tukafuatilia mienendo ya maafisa wetu wanao kusanya mapato katika vyanzo mbalimbali lakini vilevile utaratibu tunao utumia kuwapata mawakala wanao kusanya mapato katika halmashauri zetu, "amesema Mhe. Kairuki.
Amesema ni imani yake kuwa wataendelea kusimamia vyema vyanzo vya mapato na ukusanyaji wake na kuhakikisha wanapata mapato halisi na makubwa zaidi ikiwa ni pamoja na kusimamia vyema mfumo wa kazi ambapo kwasasa wanahudumia kuanzaia ngazi ya vijiji hadi kata.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Wahasibu Nchini Geogre Eston Mashauri amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuangalia hesabu zilizopita na kufanya mapitio ya ufungaji wa hesabu za mwaka huu na kutatua changamoto zote ili kuhakikisha hakuna hoja inayoweza kujitokeza.
No comments:
Post a Comment