WATAALAMU 1,600 WASAJILIWA NA TUME YA TEHAMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, August 25, 2023

WATAALAMU 1,600 WASAJILIWA NA TUME YA TEHAMA

Mkurugenzi wa Tume ya TEHAMA Dkt. Nkundwe Mwasaga,akizungumza na waandishi wa habari Leo Agosti 25,2023 Jijini Dodoma,kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za TUME hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa fedha wa 2023/2024.

Na Okuly Julius-Dodoma

Mkurugenzi wa Tume ya TEHAMA Dkt. Nkundwe Mwasaga amesema hadi kufikia Juni 31 , 2023 TUME hiyo imesajili wataalam wa TEHAMA 1,600 wanaohudumia nchi nzima na bado zoezi la usajili linaendelea.


Dkt.Nkundwe ameyasema hayo leo Agosti 25,2023 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za TUME hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa fedha wa 2023/2024.

"Tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika TEHAMA kwani hapa nchini kampuni mbalimbali zimetengeneza mitaji mikubwa na zinafanya kazi nchi nyingi duniani na mpaka sasa hapa nchini tumeshawasajuli wataalamu 1,600 ambao wanafanya kazi katika maeneo mbalimbali,"amesema Dkt.Nkundwe



Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali amesema kuwa Serikali imeamua kuwekeza kwa nguvu kwenye Tanzania ya Kidijitali chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo msimamizi mkuu unafanywa na Tume ya TEHAMA.

"Hili ni jambo kubwa kwani fedha nyingi imewekezwa kwa ajili ya kuboresha TEHAMA nchini kwani shughuli mbalimbali kwa sasa duniani zinafanyika kwa njia ya kidijitali ikiwemo huduma za malipo mabalimbali, huduma za afya za matibabu, uzalishaji, kilimo, uchimbaji wa madini,"amesema Msigwa


MAFANIKIO YA TUME YA TEHAMA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2022/2023

Kuanzishwa kwa mradi wa kujengwa kituo kikubwa cha Taifa cha Ubunifu Dar Es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma kwa wataalam, watafiti, na wabunifu wa TEHAMA.


Kuanzisha kituo kimoja cha ubunifu TEHAMA (Softcentre) Zanzibar, vinne vya Kanda katika majiji ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Tanga, Lindi na Mbeya kwa ajili ya kuendeleza kampuni changa za TEHAMA na kuendeleza kituo cha Dar es Salaam ili kukuza kiwango cha uzalishaji wa bidhaa za TEHAMA na kukuza uchumi wa nchi.



Kuanzisha kituo cha kutengeneza na kuboresha vifaa vya TEHAMA (ICT refurbishment and assembly centre).

Kuwezesha mafunzo maalum ya TEHAMA kwa wataalam kukuza na kuendeleza ujuzi wa TEHAMA nchini.

Kuwezesha mijadala miwili (2) ya wadau kutoka sekta ya Umma na Binafsi inayohusu maboresho ya sheria katika sekta ya TEHAMA na kuvutia uwekezaji ili kuharakisha ukuaji wa sekta kwa kuihusisha sekta binafsi.

Mijadala ya TEHAMA na Sekta binafsi imeiwezesha Tume kusaini mikataba ya maelewano ya uwezeshaji katika TEHAMA na mashirikika na taasisi mbalimbali zikiwemo Benki ya CRDB, UNCDF, UNDP, DOT na UNESCO.

Kutengeneza mfumo jumuishi utakaounganisha usajili na uendelezaji wa wataalam na wabunifu TEHAMA nchini (ICT human capital development system): lengo la mfumo huu ni kutambua bunifu na kupanua wigo wa ukuzaji wa wabunifu na bidhaa na huduma za TEHAMA zinazozalishwa Tanzania na hivyo kukuza pato la Taifa na kuongeza fursa za ajira kupitia TEHAMA na maendeleo ya kidijitali duniani.

Kuandaa mkutano wa mwaka wa TEHAMA (TAIC) na Tuzo ya TEHAMA Tanzania (Tanzania ICT Award): Hili lilikuwa kongamano kubwa la mwaka la TEHAMA lililofanyika Zanzibar mwezi Oktoba, 2022 na kuwashirikisha wawekezaji na wadau mbalimbali wa TEHAMA kutoka ndani na nje ya nchi wapatao 1,200.

VIPAUMBELE VYA TUME YA TEHAMA KWA MWAKA 2023/2024

▫️Kuendelea na ukamilishwaji wa vituo vya ubunifu TEHAMA (Soft centers) katika Kanda 5 pamoja na kuanzisha kituo kimoja Zanzibar.

▫️Kuanzisha kituo cha kutengeneza na kuboresha vifaa vya TEHAMA (ICT Refurbishment and Assembly centre).

▫️Kuwezesha uanzishaji wa vituo vya majaribio vya ubunifu TEHAMA (District ICT Startups Innovation hubs) katika Wilaya 10.

▫️Kufanya tafiti za maendeleo ya TEHAMA nchini na kufanya tathmini ya kitaifa ya hatua za utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya TEHAMA.

▫️Kuratibu na kuandaa matukio ya kuvutia uwekezaji na kutangaza masoko ya bidhaa za TEHAMA ndani na nje ya nchi.

▫️Kushirikiana na washirika wa maendeleo na kampuni za kimataifa katika kuendeleza bunifu za TEHAMA ikiwemo kuwezesha utengenezaji wa bidhaa za TEHAMA hapa nchini.

▫️Kujenga kituo cha Artificial Intelligence kwa ajili ya kuendeleza wataalam wa TEHAMA.

▫️Kuwezesha mafunzo maalum ya wataalam wa TEHAMA 500 ili kukuza na kuendeleza ujuzi wa TEHAMA nchini.

▫️Kukuza soko la bidhaa na huduma za kampuni ndogondogo “startup” kwa kushiriki maonesho na makongamano yanayohusu fursa za startups duniani.

▫️Kuratibu na kutengeneza mfumo wa usimamizi wa utekelezaji wa Sera ya TEHAMA na kufanya tafiti za kuweza kufanya maboresho ya sera kulingana na mabadiliko ya teknolojia.

▫️Kujenga metaverse studio kwa ajili ya kutengeneza maudhui ya metaverse na pia kuboresha maudhui ya mitandao.

▫️Kufanya tafiti za maendeleo ya TEHAMA kwa kila wilaya.

▫️Kuanzisha Kituo cha Resilience Academy hapa nchini.


Majukuu makuu ya Tume ya TEHAMA ni kuratibu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya TEHAMA, katika Sekta zote binafsi na Taasisi za Serikali, Kukuza TEHAMA kwa kuwawezesha wataalam wenye uwezo katika kufanya shughuli zote zinazohusu TEHAMA nchini, pia kuifanya Tanzania kushindana kidunia katika utekelezaji shughuli za TEHAMA.

No comments:

Post a Comment