WATUMISHI TAMISEMI WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA KIUTENDAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, August 7, 2023

WATUMISHI TAMISEMI WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA KIUTENDAJI


Asila Twaha, Mbeya

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Bi. Paulina Nkwama ametoa wito kwa Watumishi wa TAMISEMI na Taasisi zake kuzingatia maadili ya utendaji kazi ili kutoa huduma bora kwa wananchi.


Bi. Paulina amesema hayo Agosti 7, 2023 alipotembelea Banda la Ofisi ya Rais TAMISEMI na Taasisi zake katika Maonesho ya Wakulima NaneNane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.


Bi. Mkwama amesema uzingatiaji wa maadili kwa watumishi wa TAMISEMI ni muhimu kwani unagusa maisha ya wananchi moja kwa moja katika eneo la utoaji wa huduma, hivyo ni wajibu wa watumishi hao kuhakikisha wanatoa huduma kwa mujibu wa Kanuni, Sheria, Taratibu na Miongozo ya kiutumishi iliyopo.


Ameongeza kuwa, utoaji wa huduma kwa kumjali mteja ni jambo la kupewa kipaumbele katika maonesho hayo kwani yanatoa fursa kwa wananchi kupata huduma kwa urahisi ikiwa ni pamoja na kutatuliwa kero na changamoto zinazowakabili.




Maonesho ya Wakulima NaneNane Kitaifa 2023 yanayoendelea Mkoani Mbeya yamebebwa na Kauli Mbiu “Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula"

No comments:

Post a Comment