Na Mwandishi Wetu, Mwanza.
Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Mhe. Dkt. Yose Mlyambina ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kutoa mafunzo ya kuwajengea uelewa wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kwa Majaji wa Mahakama pamoja na taasisi zinazohusu utatuzi wa migogoro ya kikazi katika eneo la kujenga uelewa wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.
Ametoa pongezi hizo wakati wa kikao kazi kilichoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kilichofanyika Septemba 15, 2023, Jijini Mwanza na kuhudhuliwa na Majaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi pamoja na Wakurugenzi wa CMA.
Aidha, amesema mafunzo hayo yatasaidia sana taasisi hizo kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya Sheria zinazohusu ulipaji wa fidia kwa wafanyakazi wanaoumia au kuugua wakiwa kazini.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Mhe. Thomas Malekela amesema jukumu la CMA ni kushughulikia haki zinazovunjwa mahala pa kazi na uamuzi unaotolewa na muamuzi kwa mfanyakazi kurudishwa kazini baada ya kupata mgogoro kazini inampelekea kuwa mwanachama tena wa WCF.
No comments:
Post a Comment