NAIBU WAZIRI KASEKENYA AWATAKA AQRB KUSIMAMIA UJENZI WA MAJENGO KWA UFANISI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, September 1, 2023

NAIBU WAZIRI KASEKENYA AWATAKA AQRB KUSIMAMIA UJENZI WA MAJENGO KWA UFANISI

Na,Okuly Julius,Dodoma. 

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya amesema kuwa majengo mengi yanayojengwa nchini yanajengwa chini ya kiwango kwasababu ya usimamizi usio sahihi. 


 Mhandisi Kasekenya meyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha wafanyakazi wa Bodi ya usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Nchini (AQRB), kilichofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).


 Aidha, amewataka watumishi wa Bodi ya Usajili Wa kufanya kazi kwa ushirikiano na kutatua changamoto zao katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza weledi kwenye utendaji. 


 Amesema miongoni mwa manufaa ya ushirikiano na umoja kazini ni pamoja na kuifanya taasisi kutoa huduma za viwango kwa wadau.  
 “Vikao kama hivi vinasaidia watu kuondokana na mazingira ya utendaji ya kawaida sababu mnakaa pamoja mnafahamiana vizuri kitabia, mnajitathmini na kuja na suluhu ya utatuzi wa changamoto ambazo zinakabili taasisi maana vinahusisha kila kada zote, tumieni vizuri fursa hii ‘ amesema Kasekenya. 


Akifafanua umuhimu wa kikao hicho Mha. Kasekenya amewataka watumishi wa bodi hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani mazingira ya utendaji wa taasisi ni kutoa huduma kwa watalaam wa fani ya wabunifu majengo na wakadiriaji wa majenzi. 

 
Sanjari na hayo Mha Kasekenya amesema Serikali inathamini mchango wa AQRB na inahitaji michango ya bodi katika kuwezesha na kuendelea ujenzi wa Tanzania ya viwanda kwa kusisitiza kuwepo kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wake ili wapate uzoefu na ujuzi hatimaye waweze kushindana katika soko la ndani na nje ya nchi. Kwa upande wake Katibu Mkuu, Bwa. Ludovick Nduhiye, amewapongeza AQRB kwa kuendelea kufanya vikao vya wafanyakazi na kuwataka watumishi kuhakikisha wanaeleza kwa uwazi changamoto zote wanazokutana nazo ili kuimarisha utendaji wa taasisi. 


 “Kama watumishi wa Ummamna wajibu mkubwa katika kuhakikisha majenzi yanafata viwango vinavyotakiwa kulingana na fani inavyotaka, kama wataalamu serikali inawategemea sana kwenye ushauri hususani katika kipindi hiki ambacho taasisi na wananchi wanajenga sana mji wa Dodoma”alisisitiza Bwa. Nduhiye. 


 Sambamba na hayo, Msajili wa Bodi ya usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Mbunifu Majengo Edwin John Nnunduma, ametaja vipaumbele vya bodi hiyo kuwa ni kuwajengea uwezo wataalamu wao ili kuwa na uzoefu, umaili pamoja na ujuzi kazini. "Kwa kushirikiana na wizara ya ujenzi, wizara umehuisha kipengele cha local content ili miradi mikubwa ya wizara ya ujenzi itumike kiwafundisha wataalamu na wahitimu wa vyuo vikuu ambao wanasomea tasnia hizi za ufundi,”amesema Nnunduma. 



Pia ameongeza kuwa bodi hiyo inaimarisha ufutiliaji na kutadhmini kazi pamoja na mienendo ya wataalamu wao kwa kuwapatia vitendea kazi vya kisasa.


 Nao baadhi ya washiriki wa kikao hicho wameipongeza AQRB kwa kuandaa mafunzo hayo ambapo wamesema yatawasaidia katika utendaji kazi wao na kwenda kuyafanyia kazi yale walio agizwa.

No comments:

Post a Comment