TFRA yapongezwa upatikanaji wa mbolea nchini - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 12, 2023

TFRA yapongezwa upatikanaji wa mbolea nchini


Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania(TFRA), Patrick Mwalunenge ameipongeza TFRA kwa kuhakikisha mbolea zinapatikana katika maeneo mengi nchini na kuwawezesha wakulima kufanya maandalizi kwa kununua mbolea hizo mapema.

"Nimezunguka maeneo mengi, mbolea ipo na wakulima wananunua na kuhifadhi hivyo niwapongeze sana kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya" Alisema Mwalunenge.


Mwalunenge ametoa pongezi hizo leo mara baada ya kumaliza kikao cha kamati ya Bodi ya Fedha, Mipango na Utawala kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka Jijini Dar es Salaam.

Akihitimisha kikao hicho, mwenyekiti wa kamati ya Fedha, Mipango na Utawala, Mhandisi Juma Omary Mdeke amewashukuru wajumbe wa kamati na menejimenti ya TFRA kwa kushiriki kikamilifu katika kujadili mada mbalimbali na kupokea maoni yaliyotolewa ili kuboresha utendaji na hivyo kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwenye tasnia ya mbolea.

Aidha, Mhandisi Mdeke ameitaka Menejimenti kuishirikisha bodi hiyo mambo inayokutana nayo ili kwa pamoja waone namna bora ya kuboresha tasnia hiyo na hivyo kufikia maono ya kitaifa katika kuwahudumia wakulima.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TFRA, Dkt. Stephan Ngailo amewashukuru wajumbe wa bodi na menejiment kwa ujumla kwa mawazo chanya yatakayosaidia kuboresha tasnia katika majukumu yake ya kila siku.

Kikao hicho cha siku moja ni maandalizi kuelekea kikao cha Bodi kinachotarajia kufanyika hivi karibuni ikiwa ni kwa mujibu wa miongozo na taratibu za usimamizi wa Mamlaka za Serikali.


No comments:

Post a Comment