Watumishi Waliopata Ufadhili wa DTP Watakiwa Kutumia Fursa hiyo Kikamilifu. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, September 9, 2023

Watumishi Waliopata Ufadhili wa DTP Watakiwa Kutumia Fursa hiyo Kikamilifu.


Na Okuly Julius-Dodoma

Watumishi waliopata ufadhili wa mafunzo chini ya Mradi wa Tanzania ya Kidigitali (DTP), wametakiwa kutumia fursa hiyo kikamilifu, kujifunza kwa bidii na kuwa na uelewa mzuri wa masomo watakaofundishwa ili watakaporudi waweze kuleta mabadiliko chanya yatakayo saidia kuboresha utoaji wa huduma za Serikali.


Hayo yamesemwa leo Septemba 9, 2023 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla, katika hafla ya kuwakabidhi vyeti vya ufadhili wa masomo ya muda mrefu nje ya nchi kwa watumishi wa umma wapatao 20 kutoka katika Wizara, taasisi za umma na halmashauri za miji na wilaya.


Abdulla amesema kuwa awamu ya kwanza ambayo inajumuisha watumishi 20 kati ya 211 walioomba kozi ndefu ambao kupitia kamati maalum iliyochakata na kuwapata watu hao watakaokwenda kuongeza ujuzi wa teknolojia mpya.


“Ninatoa rai kwa kila aliyepata ufadhili huu, kutumia kikamilifu fursa hii kujifunza kwa bidii na kuwa na uelewa mzuri wa masomo mtakayokuwa mkifundishwa ili mtakaporudi muweze kuleta mabadiliko chanya yatakayo saidia kuboresha utoaji wa huduma za Serikali,”amesema.


Kwa upande wake,Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Gerald Mbwafu amewataka watumishi hao kuepuka kurudishwa nchini kwa aibu kwa kwenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu za nchi na vyuo wanazokwenda masomoni.


“Tunasikitika sana tunapoona Mtanzania arudishwa nchi kwa aibu. Tujiepushe na makosa ya jinai na madai ambayo yanatokana na tamaa, utapeli na suala la dawa za kulevya,”amesema Mbwafu


Naye Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Xavier Daudi amewataka kuhakikisha kuwa wanajifunza utamaduni ambao umefikisha mataifa hayo yalipo kimaendeleo.


Naye Mwenyekiti wa kamati ya Usimamizi wa mafunzo hayo, Salome Kessy amesema watumishi wa umma kutoka katika taasisi mbalimbali 500 watapatiwa mafunzo kupitia mpango.


Salome amesema kati ya hao watumishi 50 watapatiwa mafunzo ya muda mrefu na watumishi 450 watapatiwa mafunzo ya muda mfupi kwenye maeneo yaliyobainika mapungufu ya mafunzo na ujuzi adimu wa kidigitali.


Amesema Sh11.4 bilioni zilitengwa kwenye mradi wa huo ambapo awamu ya kwanza itaanza na watalam 20 ambao watakwenda kuchukua mafunzo ya mwaka mmoja hadi miwili katika nchi za Ujerumani, Uingereza, Marekani na Malasia.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA YA WATUMISHI HAO WALIOPATA UFADHILI WA DTP WAKIPATIWA VYETI NA KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MOHAMMED KHAMIS ABDULLAH 


No comments:

Post a Comment