ZAIDI YA WATU 600 WAFARIKI NCHINI MOROCCO BAADA YA TETEMEKO LA ARDHI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, September 9, 2023

ZAIDI YA WATU 600 WAFARIKI NCHINI MOROCCO BAADA YA TETEMEKO LA ARDHI.


CHANZO BBC SWAHILI 

Tetemeko kubwa la ardhi lililotokea kusini mwa Morocco, ambalo limeua zaidi ya watu 600, limeharibu pia maeneo makubwa ya kituo cha kihistoria cha Marrakesh.

Wakazi na watalii wengi walilazimika kulala nje usiku kucha, kutokana na hofu ya kutokea kwa tetemeko la ardhi lililozidisha hali katika jiji hilo.

Idadi ya waliopoteza maisha inatarajiwa kuongezeka zaidi baada ya tetemeko la ardhi ambalo linasemekana kukumba theluthi moja ya nchi.


Ripoti zinasema changamoto kubwa ni kufikia watu katika vijiji vya mbali katika Milima ya Atlas ambavyo viliathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi.

Huenda ikachukua muda kabla ya waokoaji kufikia vijiji hivyo ambavyo vina majengo mengi ya zamani.

Hata watu katika Visiwa vya Canary karibu na pwani ya Morocco na Algeria, jirani yake wa mashariki, wanasema walihisi tetemeko hilo.

Tumeona matukio ya watu walioshtuka wakikimbia nyumba zao na kutorokea mitaa ya Marrakesh. Na tumesikia kwamba kuta za kale za jiji zimeathiriwa na tetemeko hilo pia.


WIZARA YA MAMBO YA NDANI

Sasa tunathibitisha kwamba watu 632 walikufa na 329 walijeruhiwa, kulingana na wizara ya mambo ya ndani ya Morocco, iliyonukuliwa na shirika la habari la AFP.

Kulingana na wizara hiyo, watu 51 miongoni mwa waliojeruhiwa, walikuwa katika hali mbaya baada ya tetemeko la ardhi.

Mwanahabari wa Morocco Aida Alami alikulia huko Marrakesh na amekuwa akiwasiliana na wazazi wake ambao wako huko.

Anasema tetemeko hilo halikutarajiwa kabisa "Sio nchi ambayo watu wanajua la kufanya iwapo kutakuwa na matetemeko ya ardhi na watu walikuwa nje. Walikuwa na wasiwasi sana kuhusu mitetemeko ya baadaye na hawakujua la kufanya na hakuna mtu aliyekuwa akiwaambia la kufanya," aliambia BBC.

"Baadhi ya picha za kushtua tulizoziona asubuhi ya leo [ni] za kuta za zamani ambazo ziko karibu na jiji la zamani ambazo kila mtu ambaye amekuwa Marrakesh ametembea. “Na tunaona vifusi na inaashiria uharibifu mkubwa ndani, haya ni majengo ya zamani sana, pengine hayakuwa imara vya kutosha.

CHANZO BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment