CHALAMILA ASHANGAA UJI WA MBAAZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, October 30, 2023

CHALAMILA ASHANGAA UJI WA MBAAZI


Na Andrew Chale, Dar es Salaam.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ni miongoni mwa viongozi waliobahatika kuonja uji maalum uliotengenezwa kwa zao la Mbaazi linalosimamiwa na Shirika la RIKOLTO.

RC Chalamila amepata fursa hiyo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano mkuu wa mwaka wa Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam, ambapo katika tukio hilo Afisa uhusiano wa RICOLTO,
David Minja amemfahamisha RC Chalamila namna zao hilo linavyosaidia uchumi nchini.

Ambapo amesema namna mbaazi ilivyo ina mapishi ya aina nyingi na hadi sasa wameweza kufikia mikoa mingi kwa kutoa mafunzo ya mapishi mbalimbali ya zao hilo.

Aidha, katika tukio hilo, RC Chalamila amedai ni mara ya kwanza kuunywa uji huo na kukiri utamu wake.


No comments:

Post a Comment