Na; Mwandishi Wetu, Dodoma.
Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ambayo ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeendelea kutoa elimu na kuwahasa vijana kufanya kazi kwa uweledi ili kuwa chachu ya maendeleo kwa Taifa.
Ameyasema hayo Kaimu Mkurugenzi wa Usuluhishi Mhe. Rodney Mataris leo Oktoba 2, 2023 wakati akitoa elimu kuhusu masuala ya Usuluhishi na Uamuzi kwa vijana kuelekea Maadhimisho ya Vijana Kitaifa yanayofanyika Mkoani Manyara kuanzia tarehe 8 hadi 14, Oktoba, 2023.
Aidha, amesema Uchumi wa nchi unawategemea vijana, hivyo utoaji elimu kwa nguvu kazi hiyo utasaidia kuleta usuluhishi na kutatua migogoro inayoletwa na vijana katika maeneo yao ya kazi ili warudi katika utekelezaji wa majukumu yao ya ujenzi wa maendeleo ya nchi.
Vilevile, amesema vijana wanatakiwa kujitambua na kuachana na maswala ya mahusiano katika maeneo ya kazi ambayo yanaweza kusababisha weledi na ufanisi wa utendaji kazi kushuka lakini pia kuepusha migogoro isiyo ya lazima.
No comments:
Post a Comment