Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amewahasa vijana kujitambua na kuwa wazalendo katika kulijenga Taifa lao.
Amesema maendeleo ya Taifa lolote yanahitaji vijana wanaojitambua, wanaofahamu historia ya nchi yao, wanaojali Afya zao, wakatambua wajibu wao, wakafanya kazi kwa bidii na wakawa msitari wa mbele katika kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na serikali.
Mhe. Katambi amebainisha hayo Oktoba 8, 2023 alipotembelea mabanda ya vijana wajasiliamali ikiwa ni wiki ya vijana kitaifa inayofanyika Mkoani Manyara na kukagua maendelea ya shughuli za mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2023..
Aidha, amesema Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa mazingira wezeshi na fursa za ajira kwa vijana ili kutimiza malengo waliyojiwekea ikiwa ni pamoja kutoa programu za kukuza ujuzi, mikopo kwa mtu mmoja mmoja ili wajikwamue kiuchumi.
Hata hivyo, Mhe. Katambi amekagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa Kwaraa na kuridhishwa nao ambapo amesema umefikia asilimia 95 na wapo tayari kumpokea Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge kitaifa 2023.








No comments:
Post a Comment