OR-TAMISEMI
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema Serikali katika mwaka wa fedha 2023/24 imepeleka Shilingi Bilioni 1.4 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Dkt.Dugange ameyasema hayo wakati akijibu maswali ya Wabunge katika kikao cha nane cha mkutano wa 13 wa Bunge unaoendelea jijini Dodoma.
Dkt. Dugange amesema Halmashauri inaendelea na taratibu za kupata mzabuni kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi kwenye chumba cha upasuaji wa dharura, jengo la X-ray, stoo ya kuhifadhia dawa, jengo la kliniki ya Mama na Mtoto, jengo la kufulia pamoja na kufanya ukarabati wa majengo mengine.
Aidha Mhe Dkt. Dugange amesema Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya inaendelea na uhakiki katika Hospitali za Halmashauri ili kuweza kubaini mahitaji ya vyumba vya kuhudumia watoto njiti na kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati.
No comments:
Post a Comment