Dkt. Mahera aipa kongole UCSAF kwa kuandaa mafunzo ya TEHAMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, November 27, 2023

Dkt. Mahera aipa kongole UCSAF kwa kuandaa mafunzo ya TEHAMA


Na Okuly Julius-Dodoma 

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya Dkt. Wilson Mahera ameupongeza Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kuandaa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu.


Amesema TEHAMA ni muhimu katika kukuza uchumi wa Taifa ambapo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa mabalozi wa teknolojia katika mikoa yao.


Dkt. Mahera ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).


“Mafunzo haya yasiishie kwenu ila niwaombe mhakikishe mnawafikishia na wenzenu katika shule zenu na ikiwezekana na shule za jirani ili ujuzi huu ukasaidie walimu katika katika utendaji wao wa kazi,”


Na kuongeza kuwa “vifaa mlivyokabidhiwa navyo mvitunze na msivitumie katika kazi nyingine isipokuwa lengo lililokusudiwa ka kurahisisha majukumu ya walimu katika utunzaji wa kumbukumbu kidijitali,kuchakata mitihani na matokeo ya mitihani kwa wanafunzi,”amesema Dkt. Mahera



Kwa upande wake Kaimu Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) John Sumia Munkondya amesema UCSAF imekuwa ikitoa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu kuanzia mwaka 2016/2017 huku jumla ya walimu 3465 wakiwa wamenufaika.

Amesema kwa mwaka huu wa 2023 mafunzo hayo yanahusisha walimu wa sekondari kutoka mikoa mitatu ambayo ni Tabora 16,Kigoma 16 na Songwe 10 na kufanya jumla ya walimu 42 kushiriki mafunzo hayo ya wiki moja.

 
“nitoe wito kwa walimu ambao wanapata mafunzo haya kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa kwenda kuwafundisha walimu wengine katika shule zao ili kuhakikisha elimu na ujuzi huo unawafikia na kuwanufaisha walimu pamoja na wanafunzi kwa ujumla,”amesema Munkondya

 
Pia ameongeza kuwa katika kuondoa changamoto ya mawasiliano mashuleni UCSAF imekuwa ikipeleka vifaa vya TEHAMA kama komputa,vishkwambi na vifaa vingine mashuleni na kuwafundisha walimu ambao nao wamekuwa wakiwafundisha wanafunzi.


 
Naye Kaimu Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu kutoka chuo kikuu cha Dodoma UDOM Dr. Florence Rashidi amesema kuwa kwa mwaka huu mafunzo hayo yatajikita katika ujuzi wa kutengeneza kompyuta pamoja na mifumo ya kuchakata matokeo ambayo yatarahisisha ufanyaji kazi katika kukuza sekta ya elimu.

 
“walimu watakapotoka hapa naamini watakuwa na uwezo wa kukarabati vifaa vyao vya TEHAMA kwa sababu watakuwa wameshapata mafunzo na watakuwa na uwezo wa kuchakata matokeo ya mitihani ya wanafunzi jambo amabalo litasaidia wao kuondokana na kupoteza muda mwingi kuandaa na kuchakata matokeo mitihani hiyo,”amesema Dkt.Florence


 
Nao baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo akiwemo mwalimu Ndodyabike Yotham kutoka mkoa wa Kigoma pamoja na mwalimu Elizabeth Massawe kutoka Tabora wameipongeza UCSAF kwa kuandaa mafunzo hayo huku wakisema kuwa ujuzi watakaoupata wataenda kuutumia kwa vitendo ili kutimiza lengo la mradi la kuongeza na kukuza mawasiliano hususani katika maeneo ya pembezoni.

 
“kwa pamoja tunawapongeza UCSAF kwa kutambua changamoto tunayoipitia hasa kipindi cha kuandaa mitihani na kupanga matokeo ya mitihani ya wanafunzi ambapo usiri ulikuwa mdogo sana ila kwa sasa bada ya kupata vifaa vya TEHAMA na mafunzo haya itasaidia hata kuzuia uvujaji wa mitihani na matokeo yake hivyo itaongeza ufanisi katika eneo hilo,”wamesema Walimu hao

No comments:

Post a Comment