i. Ukaguzi wa barua za Uhakiki kwa madereva wa mabasi ya abiria.
-Jumla ya Mabasi 45 yalikaguliwa kati ya hayo madereva wa magari matatu hawakuwa na barua za uhakiki wa leseni zao, leseni zao zilishikiliwa na kupewa PF.114-Production of Documents wameelekezwa kufanya uhakiki wa leseni hizo ndani ya wiki moja.
ii. Utoaji wa elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa magari binafsi na abiria pamoja na makondakta wa mabasi ya abiria
- Madereva tajwa walipewa elimu na kutakiwa kutokuwa chanzo cha huzuni na majonzi katika jamii kwa kusababisha ajali zinazoepukikaWaliaswa kuendesha magari yao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za matumizi sahihi na salama ya barabara wakati wote hususani kipindi hiki kuelekea sikukuu za mwishoni mwa mwaka.
- Abiria nao wameelimishwa na kutakiwa kupaza sauti pale wanapoona vitendo na viashiria vya uvunjivu wa sheria vikivyofanywa dereva kwa kupiga namba za simu zilizobandika kwenye mabasi yao na walizotajiwa kwa mabasi ambayo hayajabandikwa namba za Wakuu wa usalama barabarani wa Mikoa ipitiwayo na mabasi hayo.
iii. Ukaguzi wa Uzima(road worthness) wa magari na uimara wa mikanda ya Abiria
Magari yote yalikaguliwa uimara wake kwa kumtumia mkaguzi wa magari aliyeambatana na RTO PWANI CPL TOBA mikanda ya magari iliyobainika kuwa mibovu madereva wake walichukuliwa hatua na kutakiwa kwenda kuirekebisha wafikapo mwisho wa safari zao.
iv. Ukaguzi wa wingi wa abiria kwenye mabasi
-Magari yaliyogundulika kuzidisha abiria kupita kiasi yalichukuliwa hatua ya kuandikiwa faini lakini pia kuwashusha abiria hao pamoja na kondakta wa gari husika ili ahakikishe abiria aliowazidisha wanapata usafiri.
Akiwa eneo la MKATA Wilaya ya Handeni Mkoani Tangaaliweza kukagua Kamera ya Ukamataji madeni ambayo imefungwa katika eneo hilo na kuona utendaji kazi wake. Kamera hiyo ilionekana kufanya kazi vizuri. Changamoto zilizoonekana katika eneo hilo alizitolea maelekezo kwa kumtaka RTO TANGA pamoja na KAIMU DTO HANDENI kuhakikisha kuwa zinafanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na Uwepo wa REGISTER ya kuandika madeni yote yanayokamatwa na kamera husika.
Akiwa njiani kuelekea WILAYANI KOROGWE alisimama katika pointi za askari maeneo ya KITUMBI, KWA MACHALIMA, KABUKU MICHUNGWANI na SEGERA, alizungumza na askari waliokuwa katika maeneo hayo na kusisitiza mambo yafuatayo;
i. Huduma bora kwa Mteja
-Ameasisitiza kuzingatia falsafa ya huduma bora kwa kutoa huduma kwa wakati na kwa weledi.
ii. RUSHWA
- Amewaonya na kuwataka askari kutojihusisha na vitendo vya kushawishi, kuomba, na kupokea Rushwa kwa kuwa vinalifedhehesha na kulidhalilisha Jeshi kwa ujumla wake na badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia kauli mbiu ya Jeshi la Polisi.
iii. Madeni yanayotokana na Tozo za Makosa ya Barabarani
-Amewataka askari kuhakikisha kuwa ukamataji wa makosa mapya unaenda sambamba na ukusanyaji wa madeni yanayotokana na tozo hizo.
Alihimiza kuwa alau kila askari angalau akamate na kukusanya madeni mawili kwa siku.
iv. Utendaji kazi kwa weledi
- Amewataka askari kutokuwa na muhali na kuchukua hatua kwa makosa yote hatarishi yafanywayo na madereva barabarani yakiwemo ya Mwendokasi(Overspeeding) na kuyapita magari mengine mahala pasiporuhusiwa(wrong overtaking).
No comments:
Post a Comment