Na Carlos Claudio , DODOMA
Mwenyekiti wa makanisa ya Presbyterian Central Mission Of Africa (PCMA) mchungaji Hyung-Gyun Kim amesisitiza suala la utakatifu katika mambo mbalimbali kwenye ibada maalumu ya kuwekwa wakfu kwa askofu mkuu wa makanisa ya hayo Dkt. Modeyah Kabeho.
Mchungaji Kim ameyasema hayo Desemba 8,12,2023 jijini Dodoma wakati akiendesha ibada maalumu ya kuwekwa wakfu kwa askofu Modeyah Kobeho kuwa askofu mkuu wa makanisa ya PCMA Tanzania.
“Unafanya uhalifu huko nje hata kama unafanya wizi ndani ya kanisa ufahamu kuwa unaiba mali ya Mungu na ni hatari sana na nakemea hiko kitendo ingawa unajiona upo sawa kumbuka haupo sawa na kuwa muangalifu valia nguo yako vizuri kwani mpangilio wa uvaaji wa nguo kwa usahihi ni sawa na imani itokayo moyoni mwa mtu,”amesema mchungaji Kim.
Aidha ameongeza kuwa amefurahi kumsimika Askofu huyo pamoja na kufanya nae kazi kwakuwa ni mtiifu, mchapa kazi mzuri anayefanya kazi katika njia ya uaminifu na utakatifu.
Kwa upande wake askofu Modeyah Kabeho amesema lengo lao ni kuinua jamii iliyokuwa njema ambayo itasaidia taifa la Tanzania
“Tunataka kulirudisha kanisa katika maadili ya Kiungu ili mambo yote yaende sawa na ndio kazi ambayo ipo mbele yangu na nitaifanya kwa uaminifu kuandaa kanisa la watu waaminifu ambao watakuwa watii na tunajua kwamba serilaki inaomba sana kupata watu waaminifu katika kazi zao lakini bado tunakosa kwasababu maadili ya kidini yamekosekana.”
“PCMA tuna maono juu ya mambo ya kiroho na kimwili ili kusaidia jamii yetu ya watanzania na tutashugulika katika upande wa kiroho, elimu na huduma za kijamii zote pamoja na afya hayo ndio malengo yangu kuona kwamba PCMA inafikia maeneo ambayo hayajafikiwa katika huduma za kijamii tutajitahidi kufanya hivyo kama tutapata ushirikiano na serikali nitafurahi sana,”amesema mchungaji Modeyah.
Naye mchungaji Eliad Lema kupitia risala aliyoiwasilisha mbele ya mgeni rasmi Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhandisi Happiness Ngalula ametoa pongezi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake wa kuendelea kutambua huduma za kiroho kwa jamii na hivyo amependekeza makao makuu ya kanisa la PCMA lililosajiliwa rasmi hapa Tanzania mwaka 1995 kuwa Jijini Dodoma ambapo ujenzi wake umefikia 75%.
No comments:
Post a Comment