HAZINA SACCOS YATOA MSAADA WA VITIMWENDO KWA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, December 8, 2023

HAZINA SACCOS YATOA MSAADA WA VITIMWENDO KWA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA

Mwenyekiti wa Bodi ya Hazina Saccoss Bw. Afrikar Tonono (kushoto), akikabidhi viti mwendo 15 kwa Kaimu Mkurugenzi Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Kessy Shija, ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii. Makabidhiano hayo yamefanyika hospitalini hapo jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma

KATIKA kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo Hazina ‘Hazina Saccos’ kimetoa msaada wa vitimwendo 15 kwa Hospitali ya Benjamini Mkapa(BMH) vyenye thamani ya sh. milioni tano.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Leo Disemba 8,2023 jijini Dodoma , Mtendaji Mkuu wa Hazina Saccos, Festo Mwaipaja amesema Saccos hiyo imechagua kupeleka viti mwendo hivyo baada ya kupokea Ombi kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa.


“Kwa kuzingatia mahitaji muhimu katika jamii, viti hivi vitasaidia wazee wasio na uwezo wa kutembea, hivyo sisi kama Hazina Saccos tunashughulika na maradhi yaliyopo katika jamii inayotuzunguka hususani wazee wasio na uwezo wa kutembea maana hayati Mwalimu Julias Nyerere alipambana na Ujinga, Maradhi na Umasikini,”amesema Mwaipaja.

Ametoa wito kwa watumishi wa umma kujiunga na Saccos hiyo huku akisisitiza kuwa wataendelea kuhudumia jamii inayowazunguka kwa kutoa misaada mbalimbali muhimu.

Uongozi wa Hazina Saccos ukiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, baada ya kuhitimisha zoezi la kukabidhi viti mwendo 15 kwa Hospitali hiyo jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk. Kessy Shija aliishukuru Saccos hiyo kwa kutoa msaada huo wa viti mwendo huku akieleza uhitaji wake bado ni mkubwa.

“Viti hivi vinahitajika sana, mahitaji ni makubwa maana hii ni hospitali ya Kanda na inatoa huduma nyingi za kibingwa na inatibu magonjwa makubwa, wazee wanatumia viti kwenda maeneo mbalimbali kupata huduma wanapofika hapa,”alisema.

Amesema hospitali hiyo kwa sasa inahudumia wagonjwa 800 kwa siku na kwamba licha ya uwepo wa viti hivyo ni vichache na mahitaji yamekuwa yakiongezeka ambapo hadi jana vimefika 75 hivyo wanahitaji vingine kama 100.


“Hivi viti mwendo ni kwa ajili ya hospitali, hivyo natoa wito kww wananchi watumie wakiwa eneo la hospitali si vinginevyo, wanaotaka kwenda navyo nje ya hapa inabidi walete maombi kwa uongozi wa hospitali ili tuangalie cha kufanya,”amesema Dk. Shija.

No comments:

Post a Comment