MRADI WA E4D UMECHOCHEA UJUZI NA AJIRA KWA VIJANA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, December 18, 2023

MRADI WA E4D UMECHOCHEA UJUZI NA AJIRA KWA VIJANA.


Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema, Mradi wa ujuzi na ajira kwa maendeleo (E4D) umeendelea kuchochea ujuzi na Ajira kwa vijana kwa kutoa mafunzo ya ufundi stadi na kuunga mkono juhudi za serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Amesema hayo Disemba 15, 2023 wakati wa mahafali ya wahitimu ya mafunzo ya muda mrefu, muda mfupi na mradi wa ujuzi na ajira kwa maendeleo E4D katika chuo cha Ufundi Stadi na Huduma Jijini Dodoma.


Aidha Prof. Ndalichako amesema mradi wa E4D umeendelea kusaidia kupiga hatua kwa haraka kwa kuunganisha serikali na wahisani wa maendeleo.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Disemba 15, 2023 katika mahafali ya chuo hicho Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment