Na Okuly Julius-Dodoma
Waziri Mchengerwa amebainisha hayo leo Disemba 19,2023 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo amesema mamlaka ya serikali za Mitaa ina jumla ya wanasheria 307 ambao ni wataalam wa Sheria na kuiomba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwaongezea nguvu ili kupata sheria ndogo na kanuni zitakazowasaidia wananchi.
Katika hatua nyingine Waziri huyo ameahidi kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhakikisha Ofisi za Wananasheria wa Serikali zinajengwa kwanzia ngazi ya Halmashauri.
"Nitatoa maelekezo mara baada ya kikao changu na wewe Mwanasheria Mkuu ambapo nitamjumuisha pia katibu Mkuu wa OR-TAMISEMI katika kikao hicho ili tuweze kuona ni ukanda gani tuanze kujenge Ofisi za Wananasheria wa Serikali ikiwezekana kwa kutumia Bajeti za ndani ya Halmashauri Kwa sababu naamini fedha zipo kama tumeweza kujenga Shule,Vituo vya Afya sasa iweje tushindwe kuwajengea Ofisi za Kisasa wanasheria wetu," amehoji Mchengerwa
Hata hivyo, Mhe.Mchengerwa amesema kuwa tatizo la ukosefu wa vyombo vya usafiri ataifikisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan ili kuona ni jinsi gani italifanyia kazi.
Pia Waziri Mchengerwa amewataka watumishi wa umma katika mamlaka ya Serikali za Mitaa kuzingatia weledi kanuni na maadili ya Utumishi kwa mustakabali wa taifa
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt. Eliezer Felesh amesema lengo la kuitisha baraza hilo ni kuandaa mpango kazi wa utekelezaji wa bajeti na kujadili hoja zinazotokana na utekelezaji wa bajeti.
Amesema mkutano huo ni wa kwanza katika mwaka huu wa fedha ambapo ajenda kuu ni utekelezaji wa bajeti na taarifa za hesabu za mwaka wa fedha uliopita.
“Ajenda ya mkutano huu inalenga kupima mafanikio ya utekelezaji wa bajeti na mizania ya bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 ambapo wajumbe watapata fursa ya kuchangia na kujadili hoja mbalimbali na kutoa mapendekezo ambayo yatawasilishwa katika mamlaka husika kwa ajiliyakufanyiwa kazi,”alisema
Aliongeza kuwa:”Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ilifanikiwa kuajiri watumishi 50 na kufanya kuwa 292.
Dkt. Felesh alisema hadi sasa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali inaupungufu wa watumishi 285 sawa na asilia 65 hivyo jitihada za kuongeza watumishi zinaendelea.
No comments:
Post a Comment