WASIRI WA POLISI WAPEWE ULINZI KUEPUSHA MIGOGORO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, December 21, 2023

WASIRI WA POLISI WAPEWE ULINZI KUEPUSHA MIGOGORO


Wafanya biashara wa soko la Majengo Jijini Dodoma wameliomba Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuwahakikishia usalama wa raia wema wanao toa siri za wahalifu ili kuepusha migogoro katika jamii na kuimarisha jitihada za ulinzi.

Kauli hiyo imetolewa Disemba 21, 2023 na wafanyabiashara hao katika mkutano wa hadhara Kati yao na watendaji wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma ambao ulikuwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea ufumbuzi.

Moja ya kero ambayo imewasilishwa ni pamoja na kulitaka Jeshi la Polisi kuongeza ulinzi katika soko hilo hususani kipindi hiki cha sikukuu kutokana na wateja wengi kufika katika soko hilo kwa ajili ya kununua mahitaji mbalimbali pamoja na kuwadhibiti vijana ambao wamekuwa wakiwasaidia wateja kubeba mizigo na kuwaibia.


Kwa upande wake Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Dodoma Kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) Israel Makongo ambayo ni mgeni rasmi katika mkutano huo amewahakikishia wafanyabiashara hao suala la ulinzi na usalama wa mali zao kwani Jeshi limejipanga vyema katika kudhibiti uhalifu kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Vile vile Makongo amewataka wafanya biashara hao pamoja na wananchi walio hudhuria mkutano huo kujitafakari kila mmoja kwa nafasi aliyopo na kutii sheria bila shuruti.

Aidha Mkuu wa Polisi jamii Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Eva Stesheni amewataka wafanya biashara hao kutumia miradi iliyoanzishwa na Jeshi la Polisi ikiwemo ulinzi jirani, ulinzi shirikishi, pamoja na Polisi kata ili kudhibiti uhalifu.

Pia mwenyekiti wa umoja wa wafanya biashara wa soko la majengo amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuwa karibu na wananchi na kusikiliza kero zao pamoja na kuzitatua.

Toka dawati la habari Dodoma.

No comments:

Post a Comment