Na Mwandishi Wetu Dar Es Salaam
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma imezichangia timu ya Taifa za Tanzania 5m/- katika harambee iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa timu za Taifa ni zinazowakilisha Tanzania ni timu ya wanaume ya mpira wa miguu, Taifa Stars, inayoshiriki Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yanayoanza Jumamosi hii nchini Ivory Coast.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt Alphonce Chandika, amesema katika hafla hiyo ya kuchangia Taifa Stars kuwa ni muhimu kuwaunga mkono mashujaa wa nchi katika kipindi hiki wanapoliwakilisha Taifa.
"BMH pia inapoichangia timu za Taifa za Tanzania inakuwa imehamasisha pia michezo kwa kuwa michezo ni Afya na unapo shiriki michezo unaondoa uwezeka kupata magonjwa yasiyo yakuambukiza," alisema Dkt Chandika.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ya harambee kuchangia timu za Taifa alikuwa alikuwa Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



No comments:
Post a Comment