Na Manase Madelemu , DODOMA
Hayo yameelezwa Januari 30,2024 jijini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt.Pindi Chana wakati akikabidhi vifaa vya TEHAMA kwa taasisi za haki jinai.
"Masuala ya sheria ni vizuri wananchi no wakayajua, uendeshaji wa kesi,upatikanaji wa nyaraka za kesi na ushahidi hukumu na maamuzi ya kesi na uwepo wa vyombo vya utoaji haki katika ngazi za jamii"Amesema
Aidha amesema serikali imejidhatiti katika kuimarisha masuala ya utoaji na upatikanaji wa haki nchini
"Kama alivosema katibu Mkuu unapochelewesha haki ni kama mtu ananyimwa haki,nisingependa tuwe wacheleweshaji wa haki hizo"
Hata hivyo ameongeza kuwa taasisi za haki jinai zimejenga mifumo mizuri ya TEHAMA ambayo inarahisisha upatikanaji wa taarifa na huduma za kisheria kwa wananchi,kwa Wakati bila urasimu na kuepusha rushwa.
"Uwepo wa mifumo ya TEHAMA na matumizi ya teknologia utawapunguzia wananchi muda na gharama za kushughulikia masuala ya kisheria na badala yake watajikita zaidi katika shughuli za Kiuchumi na maendeleo"
Awali akimkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Mary Makondo ameeleza Kuwa mradi huu umelenga kuimarisha matumizi na fursa za TEHAMA nchini ili kurahisisha upatikanaji wa haki
Pia kuimarika kwa matumizi ya TEHAMA kunawezesha kuziunganisha taasisi za haki jinai katika mfumo mmoja wa kielectronic katika kuwasiliana kiutendaji na hivyo kuimarisha ubora na upatikanaji wa huduma za kisheria zinazotolewa na taasisi hizi
"Tangu kuanziashwa kwa mfumo huu Kazi zifuatazo zimetekelezwa ikiwa ni pamoja na upembuzi yakinifu wa mahitaji ya sekta ya sheria pamoja na haki jinai kuelekea haki mtandao,vile vile ujenzi wa miundombinu ya TEHAMA kwenye jengo la Wizara"Amesema
Aidha ameeleza Kuwa Wizara inaendelea kutumia fursa ya TEHAMA kwa kushirikiana na taasisi za serikali pamoja na wadau katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Mashitaka nchini(DPP) Sylvester Mwakitalu akitoa salaam fupi za ofisi yake amesema ofisi ya Mashitaka imefarijika kupokea vifaa hivyo na vitawasaidia katika kuboresha utendaji wao wa kazi na katika kuwahudumia watanzania
Aidha tunaamini vifaa hivi vitatusaidia katika kuhakikisha kwamba haki za wananchi tunaowahudumia zinapatikana kwa wakati.
Naye Mkuu wa Gereza la Msalato SSP Flavian Justine ameeleza Kuwa vifaa hivyo kwao ni muhimu kwa kuhifadhi taarifa za wahalifu,lakini pia kwa kurahisisha taarifa za mawasiliano kati ya magereza na mahakama na kuipunguzia serikali gharama za kusafirisha wahalifu kuhudhuria mahakamani.
No comments:
Post a Comment