Ni zaidi ya miaka minne sasa tangu kijana LIZIKI DOMINICO LAURENT alipomaliza Elimu yake ya shahada ya JIOGRAFIA NA MASOMO YA MAZINGIRA kutoka chuo kikuu Cha Dodoma (UDOM).
Kama ilivyokawaida kwamba masomo siyo rahisi kijana huyu alipambana sana kuhakikisha anafikia malengo yake. Kusoma na kupata Elimu ni muhimu sana katika maisha ya binadamu na ndo chanzo Cha Maendeleo ya jamii nzima kijana Liziki aliamini.
Na hili ndilo jambo ambalo halipaswi kupuuzwa na mtu yeyote ulimwenguni.
Kila mtu anajivunia hatua kubwa na Bora Zaidi katika maisha yake, kamwe hakuna mtu asiyependa kuishi katika mazingira Safi na salama kama sheria za nchi zinavyoandikwa na Sote tunajivunia hatua hii. Na ingawa tumeshuhudia mabadiliko mengi na mazuri kimazingira, kuna hatua zaidi ambazo zinapaswa kuchukuliwa ili kuboresha hatua hizi, kwa kuwa tumeendelea kuona uchafuzi na uharibifu wa mazingira uliokithiri na unaotokana na shughuli za binadamu zisizofata na kujali umuhimu wa kuthamini mazingira. Bado tunalo hitaji kubwa la kuendelea kutoa elimu na kusimamia Uhifadhi wa mazingira nchini na duniani kutokana na aina zingine za uharibifu wa kimazingira kama matumizi ya plaskiti kama chupa za maji, mirija, mifuko na nyinginezo; plastiki ambazo zinatumika mara moja tu.
Kijana Liziki Dominico ameona jambo hili kuwa Ni jambo la busara kwake na kuamua KUANZISHA kikundi cha MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT Kwa lengo la kusaidiana katika shughuli za kuhakikisha kuwa mazingira ya nchi yanabakia kuwa Safi na salama. kupiga marufuku aina fulani za plastiki. Hata hivyo, tusisahau kuwa wakati mwingi uchafuzi na uharibifu wa mazingira unasababishwa na binadamu mwenyewe. Viwanda vinaendelea Kuzalisha plastiki ambazo hubebwa na upepo na pia kusafirishwa na maji ya mvua na mito hadi maeneo hayo.
Hivi karibuni tumeshuhudia madhara makubwa yaliyotokana na ukosefu wa Elimu ya kimazingira, watu wameathirika sana na mvua Kwa kusombwa na MAFURIKO ya maji, maporomoko mwishoni mwa mwaka 2023 ikiwa tutatoa Elimu thabiti ya kimazingira na kudhibiti uchafu huu wa plastiki ninaamini kazi utakuwa imetimika na tutaanza kufurahia matumda mazuri kutoka kwenye mazingira yetu
Tunaposherehekea siku ya Mazingira Duniani mwaka huu, tunapaswa kutambua kwamba, kamwe hatuwezi kuishi duniani peke yetu, inatubidi tufikiri kwamba kama dunia hhi ingeharibiwa kabla hatujazaliwa leo tusingeishi au tusingefurahia Mazingira mazuri tunayoyatembelea. Tunahititaji ushirikiano baina yetu na viumbe wote. Kila kiumbe kina umuhimu wake hapa duniani na kinapaswa kutunza na kuthaminiwa Kwa hali na Mali.
Ni jambo la kusitaabisha, kukwaza Hadi kutia hofu tunapowaona wawindaji haramu wakiwaua wanyama wa porini ili wajinufaishe wenyewe. Hali kama hii itaweza kuhatarisha dunia kutokana na wachache wetu kutokuwa waaminigu kwa viumbe wenzao, tunapaswa kuchukulia viumbe wengine kama viumbe wenzetu katika ikolojia. Kwa asilimia Kikubwa naungana na wataalamu wengine kusema kwamba baadhi ya magonjwa yanatokea Kwa viumbe wengine wa porini.
Na ikiwa basi tutaishi bila kuingiliana na hao wanyama wa porini maradhi ibuka yatakoma, Ni sharti na linapaswa kuchukuliwa kama nia na kusudi la Kila binadamu Kushiriki katika kutunza mazingira kwa hali na mali. La sivyo, tutaendelea kuteseka kutokana na mikurupuko ya magonjwa ambayo hayaeleweki.
Adhabu Kali za Uharibifu wa mazingira zinapaswa kutolewa pasipo huruma yeyote ili kulinda na kunusuru viumbe katika ikolojia. Shughuli za uharibifu ambao unahatarisha viumbe hai unastahili kuchukuliwa kama makosa makubwa dhidi ya wanadamu na viumbe wengine. Wazo na maoni yangu Mimi LIZIKI DOMINICO ni kwamba utii wa sheria za mazingira inaweza kuwa ndilo jambo kubwa la lufanikisha lengo la juu kabisa la mazingira Safi na salama.
Shughuli za maendeleo ni muhimu sana kwa kila nchi na mwananchi wake lakini, zahitaji kutumia njia safi na salama na ambazo hazidhuru mazingira kiwango cha kuhatarisha binadamu na viumbe wengine katika ikolojia. Shughuli za kilimo kanfo ya vyanzo vya maji, ukataji wa miti ovyo, uchimbaji wa madini usiofuata sheria za mazingira, uchomaji taka za plastiki umeonekana kuchangia Kwa kiasi Kikubwa uharibifu wa mazingira na kusababisha milipuko ya maradhi ya vifua, maradhi ya moyo na hata saratani Kwa binadamu
Mimi LIZIKI nipende kupongeza baadhi ya watu binafsi, makundi na mashirika ambayo yameamua kutumika katika kuhifadhi na kulinda mazingira yetu. Shukrani zangu za dhati ziendee mashirika na watu wote mnaojihusisha kuzoa taka za plastiki katika mazingira na kuzigeuza kuunda vitu vyenye thamani. Hii njia ni nzuri sana Kwa kulinda mazingira na endeleeni hivo ivo.
LIZIKI DOMINICO, Mwanaharakati wa Mazingira na JUKUMU LA KUHIFADHI MAZINGIRA: MWANZA ENVIRONMENT CONSTRUCTION UNIT
JUKUMU MADHUBUTI LA MECU
KUTOA ELIMU YA MAZINGIRA, KUOTESHA, KUPANDA MITI NA MAUA KUENDELEZA MISITU KATIKA MKOA WA MWANZA KWA AJILI YA KULINDA NA KUHIFADHI MAZINGIRA, KUONGEZA MAZAO YA MISITU, KUONGEZA UFANISI KATIKA MATUMIZI ENDELEVU YA RASILIMALI MISITU MAJI, HEWA NA KUBORESHA MAISHA YA MTANZANIA KUTOKANA NA UHIFADHI WA MAZINGIRA KWA KIZAZI KILICHOPO NA KIJACHO
ASASI YA MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT
JINA LA ASASI: MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT (MECU) S.L.P 1213, MWANZA. Simu: 0745901559
LIZIKI DOMINICO LAURENT, ni kijana mwenye taaluma ya mazingira kutoka chuo kikuu Cha Dodoma, Mwanamazingira na mhamasishaji wa masuala ya ikolojia, Ni mwenyekiti wa kikundi cha MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT. ana Shahada ya JIOGRAFIA NA MASOMO YA MAZINGIRA. Ni mfano wa vijana na kielelezo katika ubunifu na uhamasishaji wa jamii katika miradi ya Mazingira na kudhibiti mabadiliko ya Tabia nchi.
MAHALI KIKUNDI KILIPO
Kikundi Cha MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT kina Makao makuu yake katika Mtaa wa SWEYA beach, kata ya LUCHELELE. Wilaya ya Nyamagana Jiji la Mwanza nchini Tanzania.
MAENEO NA SHUGHULI ZA KIKUNDI
Kikundi Cha MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT (MECU) Kunajihusisha na shughuli za kuhakikisha kuwa mipanngo na malengo ya Taifa ya milenia yahusuyo Uhifadhi wa Mazingira yanafikiwa. Shughuli hizo ni kama vile
Kutoa elimu kwa wanavikundi na Kuboresha vitalu vya kuoteshea miche kwa kununua vitendea kazi.
Kutoa Elimu ya usafi na Uhifadhi wa Mazingira Kwa Kuzalisha au kuotesha Maua na miti kwenye vitalu.
Kupanda Maua na miti ya kivuli kwenye maeneo ya bustani katika sehemu mbalimbali
Kupalilia Maua, kukata na kupunguza matawi miti ya Maua
Kufyeka ukoka kwenye Maua yaliyopandwa
Kuweka mbolea kwenye Maua yaliyopandwa ili kuyafanya kustawi vizuri
Kuanzisha clubs na vyama vya kimazingira mashuleni, vyuoni na mitaani.
Kutoa Elimu ya kujikinga na magonjwa ya milipuko
Kuelimisha umma juu ya matumizi Sahihi na endelevu juu ya utumiaji wa rasilimali kama vile maji, misitu, ardhi n.k
Kukusanya taka ngumu Kwa Kufanya usafi wa maeneo mbalimbali katika maeneo mbalimbali kama vile mashuleni, vyuoni, viwandani, sokoni, Kufyeka Mazingira yote yanayozunguka Ofisi na majengo mbalimbali
Kuanzisha na Kutunza vituo vya taka ngumu (skip backets)
Kusafisha mifereji ya maji machafu
OMBI KWA WADAU, MASHIRIKA NA TAASISI
Kiikundi cha MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT kinachojihusidha na utunzaji na Uhifadhi wa Mazingira jijini Mwanza. Kikundi hiki ni Cha hiari na kipo katika kata ya LUCHELELE wilayani Nyamagana. Madhumuni ya kikundi ni Kusaidia na Kushiriki katika shughuli za Uhifadhi wa Mazingira, Kushirikiana na kusaidiana wakati wa shida na raha.nk,
Kikundi Cha MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT (MECU) kinajiendesha Kwa michango ya wanakikundi hali amabayp inaleta ugumu katika kutekeleza KAZI na majukumu yake. Ikiwa ni tamanio la Kila binadamu kuhitaji kuishi katika Mazingira Safi na salama kikundi kinaarika na kuomba wadau wa Maendeleo, hasasi za serikali na mashirika mbalimbali kukifadhiri na kukiwezesha ili kuisaidia kikundi kutekeleza majukumu yake ya Uhifadhi wa mazingira.
OMBI KWENU
Wadau wa mazingira, Asasi zingine, mashirika ya umma na binafsi pamoja na watu binafsi Kwa unyenyekevu mkubwa naomba mlipokee ombi langu Kama lilivotajwa hapo juu,
Mimi ni kijana mwenye juhudi ya kazi, sifa njema, mtii wa sheria na mwenendo unaokubalika na jamii. Ninaipenda nchi yangu na ndiyo maana natambua umuhimu wa kulinda mazingira yake imenilazimu kuchukua hatua ya kuwaombeni mawazo yenu, misaada yenu ya hali na Mali, vifaa na vitu vingine ili kusaidia kuendelea mapambano ya uhamasishaji wa Uhifadhi wa mazingira nchini. Nia yenu thabiti ndio tegemeo langu pekee.
Mwishowe nitumie fursa hii kupongeza na kuomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mheshimwa Rais wake kuendelea na KAZI nzuri ya usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira nchini.
Natanguliza shukrani zangu
LIZIKI DOMINICO LAURENT - mwenyekiti wa kikundi cha MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT na Mwanaharakati wa Mazingira
Uwezeshwaji unaoombwa:
S/No
MAHITAJI
IDADI
1. Uwezeshwaji wa vifaa vya usafi kama mafyekeo, leki, majembe na mifagio
2. Uwezeshwaji wa nauli, chakula na chai tunapotembelea taasisi zaa shule kutoa elimu ya kimazingira
3. Vitabu, vipeperushi na matini yanayohusu Elimu ya mazingira
4. Kompyuta Kwa ajili ya kuandalia na kutunzia taarifa za kikundi
5 . Vifaa vya kiofisi kama faili, kalamu, karatasi
6 . Meza na viti vya Ofisi
MECU imelenga Kuwezesha wawakilishi wa vikundi vinavyosimamia vitalu vya kuotesha miti kupata mafunzo ya namna ya kuotesha mbegu na kuhudumia miche. mpaka kufikia hatua ya kupandwa pamoja na mafunzo ya uhifadhi misitu na mazingira kwa ujumla. Pia kununua baadhi ya vitendea kazi vya bustani.
Kwa upande mwenyekiti wa MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT anakaribisha wadau wa Maendeleo kusaidia katika Kubuni na kutekeleza shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi Kwa lengo la kujitengenezea kipato, mwenyekiti anaamini kuwa kupitia kuwezeshana kifedha katika shughuli za kikundi kwa masharti pamoja na Kuhamasisha ushirikiano na watu wenye mahitaji maalumu baina yao na wanakikundi kama ulemavu, uzee, yatima, uathirika wa ukimwi na watoto wa mitaani.
Aina ya uwezeshwaji unaoombwa:
Mdau, mtu binafsi, makampuni, mashirika ya umma na binafsi ASASI zingine pamoja na wanaharakati wengine mnaombwa Kwa hali na Mali michango, mawazo, pamoja na maoni yenu katika kuhakikisha kuwa mipanngo ya kikundi cha MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT kinafanya miradi ya uelimishaji umma kuhusu mazingira Safi na salama.
Ikiwa kikundi kitapata Gharama za semina kama usafiri kwa wanasemina na wawezeshaji, chakula na chai, malazi na kununua vitendea kazi vya Uhifadhi wa Mazingira basi kikundi kitaweza kuyarudusha mazingira ya Jiji la mwanza katika hali yake ya asili.
Mantiki na uthibitisho wa kuwa na Mradi
Hivi karibuni tumeshudua uchafuzi na uharibifu wa mazingira uliokithiri. Uharibifu huo umesababisha shida na balaa nyingi Katika maisha ya Mtanzania na duniani kote.
Hata hivyo sasa siyo wakati wa kutafuta au kumlaumu aliyesababisha uharibifu ni wakati sasa wa kuanza kuchukua hatua ili kupunguza dhaama na hali mbaya ya uharibifu wa Mazingira unaoendelea Katika miongo ya hivi karibuni. Miaka hii ya 2000 kumekuwa na uharibifu mkubwa wa misitu katika wilaya nyingi hapa kwetu Tanzania uliosababishwa na ukataji ovyo wa miti, matumizi mabaya ya ardhi, ufyekwaji na uchomwaji wa misitu kwa ajili ya kilimo na ukataji wa miti ovyo kwa ajili ya kuni na mkaa.
Hali hii imesababishwa na elimu duni katika jamii kuhusu umuhimu wa kutunza misitu na mazingira kwa ujumla. Pia ukosefu wa maji, mavuno ya kutosha ya mazao ya chakula, biashara pamoja na mazao ya misitu ni miongoni mwa matokeo hasi yanayoikabili jamii ya Tanzania kutokana na uharibifu huo wa misitu na mazingira.
Kutokana na changamoto hii, kijana wa kitanzania ndgugu Liziki Dominico ameamua kuchukua hatua ya Kuhamasisha vijana wenzake kuunda kikundi cha MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT (MECU). kinachojihusisha na Uhifadhi wa mazingira jijini mwanza, taasisi ya MECU imeanza kubuni miradi mbalimbali na kuitkelekeleza ili kuinuthuru hii dunia. ilianzisha mradi wa kutoa Elimu Kwa wanafunzi mashuleni, kutoa Elimu Kwa vikundi vinavyojihusisha na mazingira, kutembelea na kuotesha na kupanda miti katika maeneo mbalimbali n.k.
MECU inaamini Miradi hii inaweza kuisaidia jamii ya kitanzania kufikia malengo ya milenia yahusiyo mazingira Safi na salama. MECU imelenga kupanda miti kwa wingi ili kulifanya Jiji la Mwanza kuwa ya kijani kwa ajili ya kuongeza mazao ya misitu na kuongeza ufanisi katika matumizi ya mazao ya misitu kwa kizazi kilichopo na kijacho.
Azma na madhumuni ya mradi na matokeo yanayotarajiwa
Azma ya mradii huu ni kuboresha shughuli za uoteshaji miti katika vikundi/vitalu kwa kuwapatia wawakilishi wa vikundi/vitalu elimu juu ya njia au mbinu sahihi ya uoteshaji miti na jinsi ya kuitunza mpaka kufikia katika hatua ya kupandwa. Pia watajifunza jinsi ya utunzaji wa misitu, matumizi endelevu ya rasilimali misitu na utunzaji wa mazingira kwa ujumla wake. Wawakilishi 96 kati ya wanufaikaji(wanavikundi) 4848 wa moja kwa moja watapata mafunzo hayo.
Aidha mradi huu utasaidia kuboresha vitalu vya kuoteshea miche kwa kuongeza baadhi ya vitendea kazi katika bustani husika.
Mradi utasaidia kuboresha maisha ya jamii kwa kuwapatia, elimu, ajira katika vitalu na pia ujira katika uuzaji wa miti hiyo.
Mwisho wa mradi tunatarajia kwamba, uzalishaji wa miche ya miti utaongezeka na kuboreka kutokana na elimu itakayotolewa. Pia elimu juu ya upandaji miti, utunzaji na utumiaji endelevu wa rasilimali misitu itafika kwa jamii nzima kwa ujumla kupitia wanavikundi watakaopata mafunzo. Mwisho wa mradi jamii itapata mwamko wa kupanda miti kwa wingi na kuitunza kwa ajili ya manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho.
Mbinu za kutekeleza miradi ya kikundi katika kuhifadhi mazingira na kufikia lengo
Kikundi Cha MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT kimedhamilia kufanya na kutekeleza miradi mbalimbali Kwa:-
Kuwapatia na kuwajengea viongozi wa vikundi vya kimazingira Mafunzo juu ya usimamizi wa vikundi vinavyojishughulisha na upandaji wa miti na namna ya kutekeleza sheria ndogo ndogo za misitu na mazingira.
Kuwashirikisha viongozi wa Kata zote za wilaya za Jiji la Mwanza pamoja na wataalamu wa misitu ya Jiji juu ya utekelezaji wa mradi ili kuweza kupata michango mbali mbali kutoka kwao.
Kuimarisha ushiriki wa vikundi vyote vinavyojihusisha na visivyokuwa na viongozi wataalamu wa mazingira na ikolojia pamoja na shughuli za upandaji miti.
Kushirikiana na kuongeza ushirikishaji na uongozi wa vijiji na kata kwa ajili ya kuandaa mapendekezo ya mpango wa usimamizi wa Misitu na mazingira pamoja na sheria ndogo ndogo za Misitu na mazingira.
Vichocheo Vikuu vya Mafanikio
Vifuatavyo ni vichocheo vikuu vya mafanikio.
MECU inayo mpango wa kulifanya Jiji la Mwanza kuwa la kijani kwa kujikita katika utoaji wa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa upandaji wa miti, mpaka sasa kikundi hiki kimeisaidia jamii katika upandaji wa miti zaidi, uhamasishaji katika kuwa na nia madhubuti ya kuthamini mazingira na kulinda rasilimali za nchi. MECU imelenga kuendelea na mradi wake wa kuielimisha jamii na Kuhamasisha kuhifadhi mazingira ya Jiji la mwanza.
.....ni lazima tuchukue hatua maadhubuti sana katika kuhakikisha tunarejesha hali nzuri ya mazingira kwa kupanda miti ili kuepusha hali duni ya maisha ya wanadamu ( mwenyekiti wa kikundi ndg. Liziki Dominico alisema katika moja ya vikao vya MECU). Miti ni muhimu sana katika mazingira YETU na hii inapaswa kupandwa katika taasisi mbali mbali ikiwemo familia, shule za msingi na Sekondari, Ofisi za vijiji, Zahanati na taasisi za kidini yaani Makanisa na Misiki pamoja na wananchi katika maeneo Yao ya wazi.
Kwa malengo hayo sisi wanakikundi wa MECU tungependa kuona kila kaya iliyoko Jiji la mwanza inapata uelewa juu ya umuhimu wa kupanda miti na kuitunza, jambo hili litaigeuza Jiji la mwanza kuwa la kijani na kuongeza mazao yatokanayo na misitu na pia kuondokana na hali ya ujangwa katika maeneo tofauti, milipuko ya magonjwa, na uchafuzi wa ziwa viktoria kama ilivyo sasa.
Mpango wa Uperembaji na Tathmini
Asasi ya MECU itafanya usimamizi na ufutiliaji wa karibu sana katika kipindi chote cha utekelezaji wa miradi yake ya kuhakikisha Jiji la mwanza linakuwa la kijani. Ufutiliaji utajumuisha usimamizi sahihi wa fedha ili kufikia lengo la mradi. Tathmini ya mradi itafanyika kwa parameta halisi na kulinganishwa ili kupata uwiano sahihi wa mabadiliko yaliyotokana na utekelezaji wa mradi. Mabadiliko hayo yatapimwa kwa kulinganisha parameta mbalimbali kabla na baada ya mradi kama vile ongezeko la miche bora, uelewa wa wanavikundi kuhusu elimu ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira n.k.
Mpango Endelevu wa Mafanikio ya Mradi.
Baada ya mradi wa awali wa kuelimisha jamii juu ya Uhifadhi wa mazingira kumalizika jamii ya Jiji la mwanza kwa ngazi ya Kata, Vijiji na Vitongoji kutakuwa na uelewa juu ya utunzaji wa misitu na umuhimu wa kupanda miti na kuitunza. Lakini pia mazao ya Misitu yataongezeka kwa sababu jamii itakuwa tayari ilishapata uelewa wa kutosha juu utunzaji wa misitu na umuhimu wa upandaji miti.
1.10 Malengo ya Miradi na viashiria vya utendaji wa MECU
Kutoa elimu na uelewa wa uoteshaji, utunzaji miti na mazingira kwa ujumla kwa jamii katika maeneo yatakayopandwa miti.
Kuongeza uoto wa asili utakaombatana na upatikanaji endelevu wa mazao ya misitu.
Kutoa hamasa ya matumizi endelevu ya misitu na mazao yatokanayo na misitu kama vile kufuga nyuki.
Kuongeza mazao yatokanayo na misitu kwa ajili ya kunyanyua kipato kwa jamii..
1.11 Matokeo yanayotarajiwa kutoka kwenye Miradi ya MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT (MECU)
Kurudisha uoto wa asili uliokuwepo siku na miaka ya nyuma na kuboresha upatikaji wa mazao ya misitu, nishati,mvua na maji.
Kuongeza kipato kwa wanajamii wa Singida Vijijini kupitia mazao ya misitu, ufugaji wa nyuki lakini pia shughuli za kilimo na ufugaji zitaboreka zaidi.
Kuweka mfumo endelevu wa wanajamii wote wa Jiji la Mwanza kwa kutunza mazingira kupitia vikundi mbalimbali kama shule, SACCOS, vijana, akina mama n.k.
Kuimarika kwa afya na kuondoa maradhi ambayo yanaweza kuzuilika kwa kuimarika kwa mazingira.
1.12 Watakaonufaika na miradi ya MECU
Kwa kuwa Kuna mahitaji mengi yahusuyo Uhifadhi na uendelelezaji wa mazingira ya Jiji la Mwanza ni muhimu kwa wananchi wote wa Wilaya zote
Wanavikundi wote zaidi ya 3500 watanufaika moja kwa moja kwa kupata elimu ya uoteshaji na utunzaji wa bustani za miti.
Wanufaikaji wasio wa moja kwa moja, hawa ni wananchi wa Wilaya ambao ndiyo watakuwa wapandaji wa miti na watanufaika kwa kuimarika kwa misitu na mazingira. Mradi wa kikundi cha MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT utaongeza upatikanaji wa maisha bora kwa wananchi wote kwa uboreshaji wa mazingira na misitu ambao utaongeza ubora wa maisha.
Kuongeza vizuizi vya upepo ambavyo kwa namna nyingine vitapunguza mmomonyoko
Kuboresha maisha/kipato cha wanajamii kwa kuuza matunda kama machungwa, maembe pamoja na mazao mengine ya misitu kwa mfano asali.
Kuongeza uelewa na ufahamu wa masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa wanajamii na kutoa mchango wa kuimarisha na kupunguza athari dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Malengo ya Mradi na viashiria vya utendaji:
Kutoa elimu na uelewa wa uoteshaji, utunzaji miti na mazingira kwa ujumla kwa jamii katika maeneo yatakayopandwa miti.
Kuongeza uoto wa asili utakaombatana na upatikanaji endelevu wa mazao ya misitu.
Kutoa hamasa ya matumizi endelevu ya misitu na mazao yatokanayo na misitu kama vile kufuga nyuki.
Kuongeza mazao yatokanayo na misitu kwa ajili ya kunyanyua kipato kwa jamii.
Mwandishi
LIZIKI DOMINICO LAURENT
Mwenyekiti wa kikundi cha MWANZA ENVIRONMENT CONSERVATION UNIT
Mwanaharakati wa Mazingira
Simu: 0745901559
Email: lizikidominico@gmail.com
No comments:
Post a Comment