Na Mwandishi Wetu, Rukwa
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ameelezea kutoridhishwa kwake na kasi ya Mkandarasi M/S Beijing Construction Engineering Group Co.Ltd.anaejenga kiwanja cha ndege cha Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Akizungumza alipokagua maendeleo ya ujenzi huo amasema Serikali imeshamlipa Mkandarasi huyo malipo ya awali hivyo kumtaka aje na mkakati wa kufidia asilimia 14.6.
Kasekenya amesema mradi huo ambao unajengwa na Serikalini kwa kushirikiana na Benki ya maendeleo ya Ulaya ulitakiwa kukamilika ndani ya muda kwani tayari Serikali ilishatoa fedha za awali na haidawi.
Naibu Waziri Kasekenya amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS kufuatilia kwa ukaribu changamoto zinazokwamisha ujenzi wa mradi huo kuweza ili kufanyiwa kazi kwa haraka kwani mradi unatakiwa kukamilika ndani ya miezi 18 kama inavyotakiwa.
"TANROADS Makao makuu,Meneja Tanroads Mkoa pamoja na Mhandisi Mshauri andaeni mpango wa utaratibu wa kuongeza vifaa, wafanyakazi na muda wa kazi ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati", amesema Kasekenya.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Rukwa Mhandisi Mgeni Mwanga, amemhakikishia Naibu Waziri wa ujenzi kwamba watashirikiana na TANROADS Makao makuu, Mshauri Mhandisi, ili kufanya kazi kwa pamoja na kufidia asilimia 14.6 ambazo mradi uko nyuma.
Vile vile Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Bw Nyakia Ally, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dakta, Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa Kiwanja cha ndege katika Mkoa wa Rukwa kwani kukamilika kwake kutarahisisha shughuli za usafarishaji na kuongeza maendeo ya kiuchumi katika mkoa huo.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi.






No comments:
Post a Comment