Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa Wa Dodoma kamishna Msaidizi Wa Polisi (ACP) Eva Stesheni ameongoza Polisi kata 18 wa Wilaya ya Dodoma Mjini na kuzifikia kaya 22 kwa lengo la kutoa elimu ya ulinzi na usalama kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza na wakazi wa mtaa wa Kikuyu kaskazini na maeneo ya jirani January 11, 2024 ACP, Stesheni amewataka wananchi wa Mkoa Wa Dodoma kujitokeza kwa wingi na kutoa ushirikiano kwa Polisi kata pindi wanapofika katika maeneo yao nakupewa elimu ya masuala ya ulinzi na usalama ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu vilivyopo katika jamii.
Aidha ACP. Stesheni amesema Jeshi la Polisi limeanzisha miradi ya Polisi jamii itakayo lenga kuisaidia jamii kuwa karibu na Jeshi lao na kutanzua vitendo vyote vya uhalifu pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo..
Ulinzi jirani, Nyumba yangu haina uhalifu ni baadhi ya miradi ya Polisi jamii hivyo jamii inapaswa kuhakikisha suala la ulinzi na usalama kuanzia ngazi ya familia linatiliwa mkazo pamoja na kutengeze kizazi kilicho bora bila kuwa na uhalifu.
ACP. stesheni amesema doria hiyo ya nyumba kwa nyumba sehemu zenye mikusanyiko pamoja kuandaa mikutano ya hadhara ya wananchi italeta tija kwa wanachi kupitia utolewaji wa elimu ya ulinzi na usalama kutoka kwa polisi kata.
Kwa upande wao wakazi wa Jiji la Dodoma wameahidi kutoa ushirikiano wa kwa Jeshi la Polisi katika kufichua wahalifu kwa kutoa taarifa.
Toka Dawati la Habari Dodoma.





No comments:
Post a Comment