Imeelezwa kuwa asilimia 49.6 ya wanawake Nchini Tanzania wanatajwa kuongoza kwa kupata maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu kutokana na shughuli mbalimbali wanazo zifanya.
Hayo yameelezwa Januari 29,2024 Jijini Dodoma na Bi Theresia Masoi ambaye ni Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakati wa MEDIA SCIENCE CAFEE ambayo imewakutanisha waandishi wa habari na wataalamu mbalimbali.
Ambapo Bi. Theresia amesema kuwa kipindupindu huashiria hali ya umaskini huku ukubwa wa tatizo la mlipuko wa ugonjwa huo likitajwa kuwakumba takribani watu million 3 mpaka 4 kwa Mwaka Duniani Kote Tanzania ikiwemo.
Pia ametaja takwimu za ugonywa huo wa Kipindupindu tangu Disemba 5 , 2023 mpaka kufikia Januari 25 ,2024 kutoka mikoa 13 ya Tanzania Bara kuwa ni wagonjwa 1299 na Vifo 31.
Mikoa hiyo ni pamoja na Mara,Dodoma ambapo Kwa sasa haipo kwenya hatari na mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Tabora,Geita,Mwanza,Katavi,Ruvuma,Simiyu, na Singida.
Naye Bwana Richard Msittu kutoka SIKIKA amezungumzia umuhimu wa kutenga Bajeti kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa mlipuko na dharura na kusema kuwa Bajeti itumike kutibu kwanza akili na Uelewa wa watu Kwa kugharamia mafunzo mbalimbali Kwa kuwawezesha wataalamu wa Afya ili waweze kufikia Jamii na kuwapa Elimu.
"Jamii inapaswa kupata Uelewa ni namna gani ya kukabiliana na magonjwa haya ya mlipuko ila jamii ielimishwe umuhimu wa kutunza Mazingira na kuzingatia Usafi wakati wote," amesema Msittu
Pia amesema madhara yanayotokana na magonjwa ya mlipuko inapunguza nguvu kazi ya Taifa na kuchelewesha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo kwani Serikali inawekeza nguvu kubwa kutibu na kupambana na madhara yanayosababishwa na magonjwa ya mlipuko Huku mengi yakisababishwa na uzembe wa Jamii kutozingatia utunzaji WA Mazingira na Usafi.
Kwa upande wake Mchumi kutoka Wizara ya Afya France Lasway amesema kuwa maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali huandaliwa Kwa mujibu wa kifungu Na. 21 Cha Sheria ya Bajeti,Sura 439 na kanuni zake za Mwaka 2015.
Pia amesema Chanjo ya ugonjwa wa Kipindupindu ipo ila Tanzania Bado haijaidhinisha kutumika kama ilivyo Kwa baadhi ya nchi zingine Duniani ikiwemo pia Malawi na baadhi ya nchi barani Africa zilizoidhinisha matumizi ya Chanjo hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA Dkt. Rose Reuben akapata wasaa wa kuilezea kwa ufupi maana ya MEDIA SCIENCE CAFEE ambayo imekuwa ikiwakutanisha waandishi wa habari na wataalamu mbalimbali .
Ambapo amesema kuwa mbali na vyanzo vingine vya milipuko ya magonjwa kama kipindupindu pia Mipango miji mibovu ni Chanzo kimojawapo Cha magonjwa hayo ya mlipuko
Dkt. Rose ametoa wito Kwa Jamii kujenga tabia ya kufanya Usafi bila kushurutishwa na wasisubirie mlipuko wa magonjwa utokee ndio wachakue hatua iwe ni tabia yao kutunza Mazingira na kuzingatia Usafi ili kupunguza athari za magonjwa hayo.
Kipindupindu unatajwa kuwa ugonjwa hatari ambao huambatana na kuharisha na kutapika huku ikielezwa kuwa ni asilimia 10 tu ya wagonjwa wanaopata kipindupindu na kulazwa hospitali huku wengine wakitembea na vimelea vya ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment