WATOA HUDUMA YA AFYA TABORA WAFUNDWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 18, 2024

WATOA HUDUMA YA AFYA TABORA WAFUNDWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO

Bi. Jesca Mugabiro Mratibu wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI akitoa mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watoa huduma za afya afya kuhusu afya ya mama na mtoto yanayolenga kusimamia uwajibikaji wa watumishi waliopo kwenye Vituo vya kutolea Huduma za Afya kwa njia ya kadi ya alama ya jamii kwenye Halmashauri na Mkoa wa Tabora.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watoa huduma za afya kuhusu afya ya mama na mtoto yanayolenga kusimamia uwajibikaji wa watumishi waliopo kwenye Vituo vya kutolea Huduma za Afya kwenye Halmashauri na Mkoa wa Tabora katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Mgeni rasmi Dkt. Honoratha Rutatinisibwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watoa huduma za afya juu ya kutathmini utoaji wa Huduma za Afya ya Mama na Mtoto kwa njia ya kadi ya alama ya jamii ili kupunguza Vifo vitokanavyo na Uzazi na Watoto Wachanga nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

OR-TAMISEMI

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatinisibwa amefungua mafunzo ya Kadi Alama (Community Score Card) ya kutathmini utoaji wa Huduma za Afya ya Mama na Mtoto ili kupunguza Vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga.

Akifungua mafunzo hayo Januari 18, 2024 mkoani humo, Dkt. Rutatinisibwa amewataka washiriki hao kushiriki kikamilifu ili kuongeza uelewa na kuboresha huduma za afya na kuondoa malalamiko kutoka kwenye jamii kwa kuwa serikali imewekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye sekta ya afya. 

Amewaasa washiriki hao kufuatilia mafunzo hayo ili kujua kadi alama ya jamii inayoruhusu jamii inayotumia huduma hizo kufanya tathmini pamoja na watoa huduma wa Kituo husika ili kubaini changamoto na kuzitafutia suluhisho kwa kushirikiana na jamii husika.

Kwa upande wake, Mratibu wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Jesca Mugabiro amesema mafunzo hayo yanalenga kusimamia uwajibikaji wa watumishi waliopo kwenye Vituo vya kutolea Huduma za Afya kwenye Halmashauri na Mkoa kwa kuwa serikali imewekeza fedha nyingi kwenye Miundombinu ya Afya, ajira na Vifaa Tiba.

Naye, Mratibu wa Elimu kwa Umma kutoka Halmashauri ya Uyui, Robert Migango ameishukuru Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Wizara ya Afya kwa kupeleka mafunzo hayo mkoani Tabora ambayo yatasaidia kusimamia huduma za afya ya mama na mtoto. 

Mradi mpya wa Tanzania Maternal and Child Health Investment Program (TMCIP) ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia (World Bank) na unalengo saidia kuboresha utoaji wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto katika Vituo vya kutolea Huduma za Afya hapa nchini kwa kutumia Kadi Alama ya Jamii ili kufanya tathmini ya Huduma husika, pia Mradi unalenga kuajiri Watumishi wa Kada mbalimbali wa Afya ambao watasaidia utoaji wa Huduma kwa jamii. Mradi huu umeanza kutekelezwa mwezi Desemba, 2022 na utatekelezwa kwa muda wa miaka Mitano hadi mwaka 2027.

No comments:

Post a Comment